Meneja wa Simba Mussa Hassan Mgosi (kulia), akiteta jambo na Kiungo wa timu hiyo Mwinyi Kazimoto baada ya kuisha mechi yao dhidi ya Jkt Ruvu,katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.
Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib (kulia),akiwania mpira na beki wa Jkt Ruvu, Nurdin Mohammed,katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchemzo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.
Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo (kulia),akivutwa jezi na beki wa Jkt Ruvu, Nurdin Mohammed,katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchemzo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.
Mashabiki wa Simba wakiwa wameduaa baada ya timu ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Jkt Ruvu, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchemzo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.
---
KOCHA msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema kuwa kikosi chake kilicheza vizuri sema mapungufu katika safu ya ushambuliaji yameinyima ushindi timu yake.
Simba imelazimishwa suluhu ya kutokufungana na JKT Ruvu katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mayanja amesema kuwa bado wanajipanga kuweza kuhakikisha wanashinda kwenye michezo yao inayofuata.
Katika mchezo wa awali Simba walitoka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Ndanda na baada ya matokeo haya wanasalia na alama nne huku kwenye michezo mingine Azam amefanikiwa kushinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea mchezo ulipigwa uwanja wa Chamazi.
Mtibwa Sugar nayo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ndanda huku Mwadui Fc wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0.
Toa Maoni Yako:
0 comments: