ASANTE MUNGU KWA KUNIPA UHAI.
Ndugu jamaa na
marafiki, naomba niwape taarifa ya ajali niliyopata barabara ya
chalinze nikiwa na dreva Patrick Ongori na rafiki yangu Mbogho Elias
tukiwa tunatoka maeneo ya msata chalinze. Tunamshukuru mungu kwa
kuendelea kutupa UHAI japo tuna maumivu ya mwili. Nimejifunza mambo
mawili katika ajali hii.
1. Nimejifunza na kuona UKUU wa Mungu katika maisha yangu. Mungu azidi kuinuliwa na kutukuzwa.
2. Nimejifunza na kuona uwepo wa KIFO mda wowote yaweza kutokea. Tujiandae kwa tukio hili la lazima.
Asante Mungu kwa kuendelea kunipa UHAI.
Zaburi 23: 1 na kuendelea ndilo andiko la faraja kwangu wakati huu mgumu.
Na Peter Sarungi.







Toa Maoni Yako:
0 comments: