Imeandikwa na Julius S. Mtatiro

Ndugu zangu, nimepokea majukumu niliyokabidhiwa na Baraza Kuu la chama changu. Siwezi kuepuka majukumu haya muhimu kwa wakati huu ambapo chama kinahitaji mchango wangu. Niko IMARA sana, natambua nimepewa majukumu wakati gani na nianze na mguu upi kwenda mbele.

Uongozi ni MZIGO na si kazi nyepesi, nahitaji kusaidiwa, kushauriwa, kuombewa na kuungwa mkono na watu wenye nia njema na siasa za mabadiliko ya kweli hapa nchini, walio ndani na nje ya CUF.

Natambua kuwa wapo wana CUF wenye sifa, uwezo, vigezo na busara kunishinda, lakini kwa sasa chama kimeona naweza kuuungana na wenzangu kukisimamia. Naahidi kuwa ntatoa uongozi wa KISASA wenye kushughulikia MASUALA. Ntatimiza wajibu wangu bila hofu yoyote kama kawaida yangu na ntatoa UONGOZI WA PAMOJA (Collective Leadership) kwa kila mwenye nia safi na CUF na mabadiliko.

Nitakuwa mhimili imara katika kipindi hiki cha mpito, kuhakikisha CUF inafanya kazi zake na inaimarika ili kujenga uwezo wa ndani, kulinda mtandao wake na kujitanua katika maeneo yote ya Bara na Zanzibar - lakini pia, ntahakikisha ushirikiano wa CUF na vyama vyote vyenye nia njema ya kupigania mabadiliko hapa Tanzania, unazidi kuimarika ili mwisho wa siku watanzania wafaidike na juhudi za mabadiliko hayo.

Mtanzania yeyote anaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa njia za ujumbe mfupi na WHATSUP kwa namba +255787536759, na Barua Pepe: juliusmtatiro@yahoo.com, na atajibiwa. Tutaendelea kuwa karibu kwa hali na mali.

Nakishukuru chama changu kwa kuniamini. Nawashukuru wanachama wote na watanzania wenzangu walionitumia salamu za pongezi ambazo sina uwezo wa kuzijibu zote.
Mungu awabariki sana.

Julius Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
The Civic United Front (CUF).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: