Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amekutana na kufanya mkutano wa kazi na watendaji wa ofisi yake ya Idara ya Mazingira kujadili kwa kina namna ya kukabiliana na hali tete ya uharibifu wa mazingira unaoendelea nchini.
Katika mkutano huo uliofanyika leo, Ikulu, Dar es salaam ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira JANUARY MAKAMBA, Makamu wa Rais ameawaagiza watendaji wa idara hiyo waache kukaa ofisini na badala yake waende kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

madhara makubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla, hivyo ni muhimu kwa
makundi yote wakiwamo wataalam wa mazingira na wadau wa maendeleo
kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema
baadhi ya watendaji wamekuwa ni sehemu ya uharibifu wa mazingira na
kuonya wataobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali ili
kukomesha tabia hiyo.

Alisema hali ya uharibifu wa mazingira ikiachwa iendelee kama ilivyo inaweza ikasababisha
Baadhi
ya watendaji waliotoa taarifa kuhusu hali ya mazingira nchini wamekiri
kuwa hali ya uharibifu wa mazingira siyo nzuri hasa kwenye mikoa ya
Dodoma, Shinyanga, Manyara, Geita, Singida na Kilimanjaro.
Inakadiriwa kuwa takribani hekta 400,000 za misitu zinaharibiwa kila mwaka hali ambayo inapelekea baadhi ya wanyama kutoweka.
Watendaji hao wameiomba serikali iongeze bajeti ya kutosha ili waweze kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi.
Makamu wa Rais ametumia siku ya mapumziko ili kujadiliana na kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini. Mkutano huo wa kazi unaendelea tena hapo kesho.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
20/8/2016




Toa Maoni Yako:
0 comments: