flydubai Boeing 737-800
---
Shirila la ndege lenye makao yake Dubai watashiriki katika maonyesho ya huduma zake nchini Uganda na Tanzania liikiangazia safari zake za bei nafuu za moja kwa moja kwenda Dubai na idadi ya safari zake zilizoongezeka
Shirika la ndege lenye makao yake Dubai, flydubai litashiriki katika maonyesho ya Utalii yatakayofanyika kwa mara ya kwanza kabisa Afrika Mashariki, litaungana na washirika wake wengine 14 kutoka Dubai katika kuonyesha huduma na vivutio mbalimbali vinavyoibukia. Flydubai imeshiriki katika maonyesho ya Kampala mnamo Agosti 24, ambapo maonyesho hayo yatahamia Dar es Salaam manamo Agosti 30.
Maonyesho haya ni fursa kwa watoa huduma wa ndani kukutana moja kwa moja na viongozi wa shirika hili na kujifunza kuhusu huduma na chaguzi ambao wasafiri wanafanya pale wanapotaka kusafiri moja kwa moja kwenda Dubai kwa ajili ya biashara au mapumziko.
Akitoa maoni yake, Issam Kazim, Mkurugenzi Mtendaji katika idara Utalii wa Dubai, alisema: “Uwezo wa Uganda na Tanzania kama soko kubwa ni mzuri, na maonyesho haya yanatupatia fursa ya kutangamana moja kwa moja na watoa huduma wa ndani na kuonyesha kile ambacho Dubai inatoa. Tunatazamia kuwa na mahusiano ya kibiashara ya muda mrefu na yenye kuzaa matunda wakati wa ziara yetu katika kukuza zaidi soko la utalii nchini Uganda kwa manufaa ya wote.”
Flydubai ilizinduliwa mwaka 2009 ili kusaidia uendeshaji wa biashara na utaliii bila vikwazo na kusaidia zaidi njozi ya Dubai kuwa kitovu cha utalii na usafiri wa anga unaotambulika kimataifa. Bidhaa za ubora wa juu, nafuu na zinazoaminika za flydubai zinazotolewa kwa madaraja yote ya biashara na ya kati, zimewawezesha watu zaidi kusafiri mara nyingi kwenda Dubai.
Sudhir Sreedharan (pichani), Anayehusika na Operesheni za Kibiashara katika flydubai (GCC, Afrika na India), alisema: “Tulifurahia sana kushiriki katika maonyesho ya kwanza ya Utalii wa Dubai kufanyika Afrika Mashariki na kuonyesha chapa Dubai na flydubai. Tumejizatiti kufungua masoko hayapati huduma na kufungua vituo ambavyo awali havikuwa au vilikuwa na safari chache za moja kwa moja kwenda Dubai. Afrika Mashariki ni soko muhimu zaidi ambalo limeonyesha ukuaji mkubwa katika miaka michache iliyopita. Kwa sasa tunafanya safari 82 kila wiki kwenda vituo 11 barani Afrika, hii inajumuisha safari 3 kwenda Entebbe na safari 4 kwenda Dar es Salaam na Zanzibar. Safari hizi za kujirudia za kila wiki zitaongezeka hadi kufikia safari 4 kwenda Entebbe na safari 7 kwenda Dar es Salaam na Zanzibar kuanzia Oktoba.”
Flydubai kwa sasa inafanya safari kwenda katika vituo 11 Afrika Kaskazini na Afrika Mashariki: Addis Ababa, Alexandria, Asmara, Dar es Salaam, Djibouti, Entebbe, Hargeisa, Juba, Khartoum, Port Sudan na Zanzibar.
Daraja la Biashara linapatikana katika njia nyingi katika mtandao wa flydubai na ndege zake hivi karibuni zimeanzisha huduma ya WiFi na Live TV kwa baadhi ya safari zake.
Shirika hili ambalo ni la pili kwa ukubwa kufanya safari za kimataifa nje ya Dubai, limejenga mtandao wa vituo 90 katika nchi 44 na hufanya safari zaidi ya 1,700 kwa wiki nje ya Dubai International (DXB), Temino namba 2 na Temino nyingine mpya iliyofunguliwa hivi karibuni Al Maktoum International- Dubai World Central (DWC).
Toa Maoni Yako:
0 comments: