Ikiwa ni takribani mwezi moja tangu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na VETA kuzindua application ijulikanayo Kama VSOMO na kuwawezesha watanzania kusoma masomo ya ufundi kupitia simu zao za Mkononi
Airtel na VETA imeendelea kutoa elimu kwa vijana na wakazi wa Dar katika maonyesho ya sabasaba ili kuhakikisha Taarifa taarifa muhimu kuhusu mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu zinawafikia watanzania wengi na kuwanufaisha vijana nchini kujisomea na kuongeza ujuzi
Mpaka sasa zaidi ya vijana 700 mkoani Dar Es saalam wameshajiandikisha na Kati yao wameshaanza kusoma kozi mbalimbali
Kwa maelezo zaidi kuhusu VSOMO tuandikie kupitia airtelfursa@tz.airtel.com
Mabalozi wa Airtel Tanzania wakitoa maelezo kwa wateja waliotembelea
banda la Airtel, juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia
simu zao za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa
kushirikiana na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Airtel Tanzania, Emmanuel Alfred akitoa maelezo juu ya
mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za mikononi
ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na Airtel
kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye
Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Veta Kilichopo Kipawa Jijini Dar es
salaam,Mhandisi Lucius Lutenganya akitoa maelezo kwa waliotembelea banda
la VETA juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao
za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana
na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa VSOMO Tanzania Gosbert Kakiziba kutoka VETA
Kipawa Jijini Dar es salaam akitoa maelezo kwa waliotembelea banda la
VETA juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya ufundi kupitia simu zao za
mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na VETA kwa kushirikiana na
Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea
kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhitimu wa Kozi ya umeme Salehe Shomari, akitoa maelezo kwa
waliotembelea banda la VETA juu ya mpango mpya wa kupata masomo ya
ufundi kupitia simu zao za mikononi ujulikanayo kama VSOMO unaotolewa na
VETA kwa kushirikiana na Airtel kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya
Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments: