1- Tunamjali sana marehemu kuliko mgonjwa au mtu alie hai.

2- Tunatumia gharama kubwa za mazishi na tunajitolea sana lakini hatujitolei kuokoa maisha ya mgonjwa.

3- Hatuna desturi ya kusafiri kwenda kuona wagonjwa lakini akifa tunaondoka ukoo mzima.

4- Watu hawakupi heshima lakini ukifa watakupa heshima za mwisho

5- Wengine hawajahi kupata kabisa zawadi za Maua lakini wakifariki yatakuja mengi sana juu ya kaburi.

6- Tunakesha hadi asubuhi kwenye msiba na ndiyo mara yetu ya kwanza kuingia chumbani kwake.

7- Hatutaki kujua kijiji chako lakini ukifa tutapanga msululu wa magari kwenda huko.

8- Tutampeleka marehemu kwenye ibada hata kama yeye mwenyewe hajawahi kuingia huko akiwa hai na alikua hana mpango na ibada.

9- Tutapamba kaburi kwa marumaru hata kama nyumba ya marehemu haikuwai kuwekewa marumaru.

10- Hatutojali kijiji kizima hakuna nyumbani iliyojengwa kwa sementi laki kaburi la marehemu litajengwa kwa sementi.

Ni mtazamo tu "Mabadiliko ya Mila" Tumekuwa na mila za kinafiki... Mila za kutukuza mauti kuliko uhai.

Lazima tujue thamani ya Maisha kuliko Kifo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: