Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mtaalam wa kutengeza mvinyo wa Dodoma Rose Erick Schlunz akiwaelezea wageni waalikwa sifa na ladha ya mvinyo huo mpya uliozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Cheers: Wageni waalikwa wakigonganisha glasi kufurahia uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro (kulia) akipita kugonganisha glasi na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa mvinyo mpya wa Dodoma Rose. Uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine Warda Kimaro (wa pili kulia) akiwamiminia wageni waalikwa mvinyo mpya wa Dodoma Rose wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
---
Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) kupitia bidhaa yake ya Dodoma Wine mwishoni mwa wiki imezindua mvinyo mpya uitwao' Dodoma Rose Wine '. Dodoma Rose ni mvinyo wenye rangi ya pink na rahisi kunywa huku ukiwa na harafu ya kuvutia ya ‘candy floss na ‘raspberry. Mvinyo huu ni unakuwa bora pale unapotumika ukiwa kwenye nyuzi 10 na ukitumia chakula chenye mwanga kidogo. Dodoma Rose inapatikana Tanzania nzima katika ujazo wa 750 ml kwa bei ya rejareja ya Tshs 10,000/-.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Bidhaa wa Dodoma Wine, Bi Warda Kimaro, alisema, "Dodoma Wine imekuja na kauli mbiu ya Onjeni ladha tofauti! Ladha tofauti si tu ya kile cha kipekee kutoka Dodoma Wine lakini pia ni wito kwa ajili ya walaji kujaribu bidhaa tofauti za Dodoma Wine na kuchangua ipi ambayo ni bora kwao. Dodoma Wine kwa sasa inapatikana katika vinywaji nne tofauti vya kipekee na vya kufurahisha; Dodoma Dry Red Wine, Dodoma Dry White Wine, Dodoma Natural Sweet Wine & leo tumezindua Dodoma Rose Wine. Dodoma Wine si tu mvinyo ambao unakidhi viwango vya Kimataifa pekee, lakini ni mvinyo wa Tanzania kuwa inatambua urithi wake ".
Bi Warda alielezea zaidi kuwa, mbali na Dodoma kuwa mji mkuu wa nchi yetu; lakini pia ndio nyumbani kwa mivinyo ya Tanzania kwa kuzalisha mvinyo wa pili mkubwa katika Afrika kusini mwa Sahara, kwa hivyo kanda hii inastahili kuwa na mvinyo wenye jina lake na ndio sababu ikaitwa Dodoma Wine kuonyesha mizizi yake na kutambua urithi wetu. Dodoma Wine ilizinduliwa 2010 Na inatengezwa kutoka kwa zabibu bora kabisa zinazolimwa na wakulima wetu wa Tanzania na hivyo kufanya kuwa kinywaji laini na tamu.
Akiongea zaidi jinsi kampuni ya TDL inavyounga mkono wakulima wa zabibu, Mkurungenzi Mtendaji wa TDL Devis Deogratius alisema, ‘Wakulima wa zabibu walikuwa na hali ngumu hapo zamani lakini kupitia miradi tumeweza kuwainua wakulima sio tu kuwapa soko la uhakika pekee, lakini pia kwa kuwapa ujuzi wa kulima zabibu kupitia mtaalamu wetu wa kutengeneza kinywaji cha Dodoma Wine Erik Schlunz, ambaye leo tuko naye hapa’.
Mtengenezaji wa kinywaji cha Dodoma Wine Erik Schlunz alipata nafasi ya kuwatembeza wangeni waalikwa na kuwapa uzoefu wa kuonja mvinyo mbali mbali ya Dodoma Wine.
Devis alimalizia kwa kuwaomba wateja kuijaribu mvinyo wa Dodoma Wine, na sana sana wakati kampeni ambazo zitakuwa zikifanyika kwenye baadhi ya bar na supermarket jijini Dar es Salaam ili kuweza kutambua ni mvinyo ngani unaowafaa. Aliongezea kuwa uzinduzi huu wa Dodoma Rose Wine ni uthibitisho wa Mafanikio yanayotokana na mvinyo wa Tanzania pamoja na wakulima wa zabibu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: