Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.
---
Pamoja na juhudi ambazo serikali imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha Watanzania wenye ualbino wanakuwa salama na amani lakini bado Tanzania inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
"Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino," alisema Ero.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.
"Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino," alisema Nyanduga..
Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.
Toa Maoni Yako:
0 comments: