Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5”leo Oktoba 12, 2015 katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga. Picha zote na Cathbert Kajuna.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney (katikati) akishangilia pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza kulia) pamoja na akiwa na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga mara baada ya uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo (wa kwanza kulia) akizungumza machache mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo, Stanslaus Mmbaga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” katika ofisi zao jijini Dar es Salaam. ambapo alisema Tembo Supaset ni matokeo ya utafiti makini uliofanywa na wataalamu wetu na imetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya soko.
Waandishi wa habari pamoja na wageni walioungana katika uzinduzi wa chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5”
---
Ikiwa ni jitihada mahususi kuwapa saruji imara zaidi wakandarasi na wafyatuaji matofali Lafarge Tanzania imezindua chapa mpya ya saruji iitwayo “Tembo Supaset 42.5” ambayo ni imara na mahususi kwa ufyatuaji matofali, zege, majengo makubwa pamoja na miradi mikubwa ya miundombinu kama madaraja, barabara na majukwaa ya michezo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney alisema kwamba Tembo Supaset 42.5 ni saruji maalum iliyobuniwa ili kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya saruji imara na inayokauka haraka katika soko la ufyatuaji matofali na zege na ujenzi mkubwa “Tembo Supaset ni matokeo ya utafiti makini uliofanywa na wataalamu wetu na imetengenezwa mahususi kukidhi mahitaji ya soko.”alisema.
Akizungumzia kuhusu maendeleo katika sekta ya ujenzi Langreney alisema kwamba kwa ujumla thamani ya sekta ya ujenzi nchini Tanzania inakadiriwa kuwa dola bilioni. Sekta hiyo ilikua kwa asilimia 7.8 mwaka 2014 na ni sawa na asilimia 8.6 ya pato la taifa ikiwa ni kutokana na ujenzi binafsi, usafirishaji na miradi mikubwa ya ujenzi. Tanzania ina idadi ya zaidi ya milioni 44 kufikia mwaka 2014 na inatarajiwa kuongezeka sambamba na ongezeko la mahitaji ya nyumba na miundombinu.”
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge Tanzania, Allan Chonjo alisema kuwa Tembo Supaset ambayo itauzwa kwenye soko la jumla na rejareja ikiwa katika ujazo wa kilo 50 ni saruji imara zaidi ikiwa na ubora kuliko saruji nyingine zilizopo kwenye soko kutokana na uimara pamoja na bei shindani ambazo zimepangwa na itakidhi mahitaji ya watumiaji kama vile:
• Kuimarika mapema jambo ambalo litawaongezea tija wazalishaji bidhaa zinazotokana na zege
• Ukaukaji wa haraka jambo litakaloyafanya matofali yaweze kuhamishika haraka na kuongeza tija wazalishaji
• Mchanganyiko mzuri wa zege na matumizi kidogo ya maji kuimarisha.
Chonjo alisema kwamba Tembo Supaset imezinduliwa ili kukidhi mahitaji ya soko kuwa na saruji imara zaidi huku akitarajia saruji hyo kupanua soko la Lafarge Tanzania hususani kwa wafyatuaji ambao hutegemea saruji inayoimarika haraka katika kazi yao. “Mbali na uimara, faida nyingine ya Supaset ni kuweza kudumu kwa muda mrefu ikiwa na maana kwamba majengo yatakayojengwa kwa saruji hiyo yatadumu zaidi”
Alisema neno Supaset linamaanisha uimara kutokana na kukauka mapema na kukaa muda mrefu zaidi katika uimara na saruji hiyo ni sehemu ya saruji za chapa ya Tembo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: