Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva  akizungumza katika mkutano na  vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mkurugenzi wa uchaguzi, Kailima Kombwey.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu,Damian Lubuva amevitaka vyama vya siasa kupeleka malalamiko yao katika kamati ya maadili ya NEC na sio kwenda kutoa malalamiko yao katika vyombo vya habari.

Lubuva aliyasema hayo jana wakati NEC ilipokutana na vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,amesema kuwa nafasi vya siasa vina nafasi ya kuhamasisha watu wapige kura kwa wale wenye sifa.
Amesema wakati wa kupiga kura watu wakipiga kura wanatakiwa kuondoka na kazi zingine zitafanywa na mawakala ndio watakaofanya kazi zoezi la kuhesabu na baadae kubandika.

Lubuva amesema watu wakikaa vituoni wanaweza kuvuruga amani na kufanya zoezi la upigaji kura kuharibika.

Amesema tume imejipanga katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na haki kutokana na mfumo wa kisasa.
Aidha amevitaka vyama vya siasa kunadi sera zao na sio kushughulika na watu kwani wananchi wanahitaji sera waweze kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi.

Baadhi ya vyama vya siasa vimeridhishwa na ushirikishwaji wa NEC katika masuala kuelekea uchaguzi mkuu na jinsi walivyojipanga uendeshashaji wa uchaguzi mkuu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: