Maelfu wa kimsikiliza Bwana Luis Farakhan 

Maadhimisho hayo yanakuja huku hasira na kauli za kutetea haki za kiraia zikiwa zinazidi kuongezeka miongoni mwa Wamarekani Wenye asili ya Kiafrika kufuatia matuko ya kuuwawa kwa vijana weusi katika mikono ya Polisi.

Makundi ya watu waliokuwa hawakupata nafasi ya kuona matukio kwenye jukwaa kuu, walilazimika kukusanyika kwenye viwambo vikubwa vya runenga ili kujionea yaliyokuwa yakitokea.

Umati huo wa watu ulikuwa na shauku ya kuwasikia wazungumzaji kwenye shughuli hiyo akiwemo kiongozi wa Jumuiya Ya Umma Wa Kiislam ya nchini Marekani (The Nation of Islam) Bwana Luis Farakhan iliyoandaa maandamano hayo chini ya kaulimbiu "Haki au Vyenginevyo"

Tukio hili linakuja kuadhimisha miaka 20 tangu kufanyika kwa maandamano ya kwanza ya aina yake yaliyoandaliwa na jumuiya hiyo mwaka 1995 yakiwa na lengo la kulalamikia dhidi ya haki za kiraia na kutoa mwamko kwa wanaume wa Kimarekani wenye asili ya Kiafrika kusimamia majukumu yao ya kisheria na kifamilia.

Umati uliofurika National Mall

Ingawaje maandamano ya mwaka huu hayakuwa na idadi kubwa ya watu kama yale ya awali, hata hivyo kiini cha malengo na fikra zake bado zilikuwa hai katika hotuba zilizotolewa jukwaani.


Wazungumzaji hao waliashiria uhusiano wa harakati za watu Weusi za kudai haki za kiraia na yale yaliyotokea katika miaka ya karibuni. Mratibu wa Kitaifa wa maandamano hayo Bi Tamika Mallory, alisoma majina ya vijana weusi waliowawa na Polisi katika miaka ya karibuni wakiwemo Tamir Rice, Michael Brown, and Eric Garner.

"Miaka 20 iliyopita, habari za kifo cha Tamir Rice zingeangukia kwenye masikio ya viziwi, na wangeachiwa Polisi kuandika ripoti za uongo badala ya kutangazwa ili ulimwengu ujue", Bi Mallory aliumbia umati wa watu uliofurika katika mji huo Mkuu wa Marekani, na kuongeza, "Mwili wa Michael Brown ungeiumiza jamii kwa majonzi badala ya kuwaamsha watu"

Maandamano hayo yaliyofanyika kwa amani, yanaukumbusha umma kuwa miaka saba tangu kuchaguliwa kwa rais wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika nchini Marekani, raia wengi wenye asili hiyo nchini humo bado hawajaridhishwa na maendeleo yaliyofikiwa katika swala la haki za kiraia.

Wakati maandamano hayo yakifanyika jijini Washington, rais Obama ambaye amekuwa akikhubiri kukhusu maswala ya udhibiti wa silaha na hali ya kutoaminiana baina ya Poilisi na jamii ya watu weusi, hakuwemo jijini humo.

Bwana Obama ambaye alikuwa katika jimbo la California akiendesha shughuli za kuchangisha fedha kwa ajili ya chama chake cha Demokrasia, yeye na mkewe waliwakilishwa kwa picha zao zilizokuwemo kwenye mikoba iliyokuwa ikiuzwa kwnye eneo la maandamano hayo lililoko karibu na Ikulu ya Marekani.

Kwa upande wake, kiongozi wa Jumuiya Ya Umma Wa Kiislam, Bw Luis Farakhan, ambaye aliandaa maanadamno ya mwanzo ya mwaka 1995, alizungumza kwa muda usiopungua masaa mawili kama alivyofanya miaka 20 iliyopita. 

Katika hotuba yake hiyo, alitoa changamoto kwa kuwataka washiriki kupiga hatua za kimaendeleo katika kiwango cha mtu binafsi pamoja na kumcha Mungu. Aidha aliikosoa serikali ya Marekani kwa kushindwa kuwalinda na kuwapa huduma bora raia khususan wale wa tabaka la chini.

"Hakuna serikali yoyote katika dunia hii, hata moja, ambayo inaweza kuwapa watu kile wanachokitaka. Watu wanataka uhuru, haki na usawa". Alisema Bwana Farakhan, na kuongeza "Munajitia tamaa bure kusubiri kitu ambacho serikali kamwe haiwezi kukupeni"

Maandamano ya jana yalihudhuriwa na vijana zaidi ikilinganishwa na mika 20 iliyopita. Ingawaje yalikuwa ya kuadhimisha "Maandamano Ya Wanaume Milioni Moja", hata hivyo idadi ya wanawake waliohudhuria mwaka huu ilikuwa kubwa zaidi kuliko ya wanaume.

Licha ya kuwa yaliandaliwa na Jumuiya ya Umma Wa Kiislam, maandmano hayo pia yalihudhuriwa na viongozi wa dini nyengine, viongozi wa Kitaifa wa taasisi na jumuiya za Wamarekani wenye asili ya Kiafrika, pamoja na wanasiasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: