Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwasenge, Jimbo la Musoma Mjini. Katika hotuba yake aliwaomba wanaMusoma kuichagua CCM ili iweze kuunda Serikali kwani imepanga kuboresha huduma mbalimbali za kijamii pamoja na ujenzi wa miundombinu eneo hilo itakayochangia kukua kwa biashara anuai.

 Alisema Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kujenga maeneo ya kisasa ya maegesho ya meli (magati) Musoma na ndani ya miezi mitatu huduma ya maji maeneo mbalimbali itapatikana kwa uhakika kutokana na kukamilika kwa mradi wa maji eneo hilo. Aliongeza pia ili kuboresha huduma za Mwisenge zahanati ya eneo hilo itabadilishwa mara moja na kuwa kituo cha afya.Kulia ni baadhi ya wasanii maharufu wa uigizaji wakishangilia wakati Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Mwisenge.Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwatambulisha baadhi ya wagombea ubunge wa Wilaya ya Tarime kwenye Mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Sirari.Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakimshangilia  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Mwisenge, Musoma Mjini.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakimshangilia  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia Mwisenge, Musoma Mjini.Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM Viwanja vya Mwisenge.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: