Mufti mkuu wa Zambia, Sheikh Assadullah Mwale akifungua kwa dua katika mkutano wa viongozi wa dini wa nchi za mashariki na kusini mwa Afrika uliofanyika leo jijini Dar.
Bi. Vanessa Anyoti kutoka YWCA Tanzania(kushoto) akizungumza kuhusiana masuala ya kijinsia pamoja na maendeleo ambayo yanaweza kupunguza maabukuzi ya virusi vya UKIMWI. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi naUtamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues
Mwenyekiti wa Mtandao wa Kimataifa wa viongozi wa dini waishio na VVU/UKIMWI na waliyoathiriwa na UKIMWI (INERELA+) Mch. Mpumzile Mabizela akizungumza na Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakirishi wa dini kutoka nchi 17 za Mashariki na Kusini mwa Afrikawakati wa mkutano ulioanza leo jijini Dar.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi naUtamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akisoma hotuba kwa Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakirishi wa dini waliofika kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania kujadili na kuweka mikakati ya kuharakisha kumalizama ambukizi mapya ya VVU/UKIMWI
Dk.Warren Namara kutoka shirika la (UNAIDS) akielezea ni kwa njia gani viongozi wa kidini wanaweza kuelimisha jamii inayowazunguka jinsi ya kupanbana na kuepuka maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Mwenyekitiwa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dk. Fatma Mrisho akitoa wito kwa mashirika mbalimbali kujikita katika utoaji wa elimu kuhusu maambukizi ya virusi vya UKIMWI huku wakishirikiana na Viongozi wa ngazi ya juu wa dini.
Baadhi ya Viongozi wa ngazi ya juu wa dini na wawakirishi wa dini kutoka nchi 17 za Mashariki na Kusini mwa Afrika wakiwa kwenye mkutano huo utakaodumu kwa takribani siku tatu.
Picha ya Pamoja Kwa washiriki walio hudhuria mkutano huo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: