Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akinadi sera zake kwa umati wa wakazi wa Mji wa Dodoma waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini humo leo Septemba 11, 2015, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu. PICHA NA OTHMAN MICHUZI, DODOMA
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa mji wa Dodoma waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Barafu mjini humo, kwa ajili ya kusikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu akiwaga cheche zake katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma.
Shangwe za nguvu wakati Chopa ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ikiwasili uwanjani hapo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alieambatana na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, wakiwasili kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: