Dj Con wa redio Efm, akiporomosha burudani ya muziki ndani ya baa ya Mawela iliyopo Sinza jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wiki wa kampeni inayoendelea ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani.
Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash (kushoto) akizungumza na mpenzi wa bia ya Tusker na mkazi wa Sinza Bw. James Lui katika baa ya Mawela iliyopo Sinza jijini Dar es salaam wakati wa kusherekea ushindi wa baa hiyo kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hiyo inatarajiwa kuifikia mikoa mingine mbalimbali Tanzania kama;- Arusha, Mbeya, Mwanza na Morogoro.
 Meneja wa bia ya Tusker SBL, Nandi Mwiyombella akikabidhi zawadi ya mfuko wenye fulana na kalamu kwa mkazi wa Sinza Bi. Zalia Ally katika hafla ya kuipongeza baa ya Mawela iliyopo Sinza jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hiyo yenye nia ya kuhamasiha baa za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye upande wa huduma inatarajiwa pia kuwafikia wakazi mbalimbali wa mikoa mingine nchini kama;- Arusha, Mbeya, Mwanza na Morogoro.
 Mkazi wa Segerea aliyetambulika kwa jina la Gaudence Mgeja pamoja na Dj wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani Dj Con wakishindana kucheza mziki kwenye hafla ya kuipongeza baa ya Havannah iliyopo Segerea mwisho jijini Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo yenye lengo la kuhamasisha kwa vitendo baa za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli inapokuja kwenye suala la huduma kwa wateja wao.
 Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Godwin Mawanja akiamsha ari ya kiwanja cha Havannah kilichopo Segerea mwisho jijini Dar wakati wa shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani linaloendeshwa na bia ya Tusker lilipotinga kwenye baa hiyo katika uhamasihaji wa kufanya kweli kwenye upande wa huduma sambamba na hilo promosheni hiyo ilikua na zawadi lukuki za fulana, bia za bure na kalamu kwa wapenzi wa bia hiyo waliofika kiwanjani hapo.
Baadhi ya wapenzi wa bia ya Tusker wakifurahia burudani ya muziki katika hafla ya kuipongeza baa ya Havannah iliyopo Segerea mwisho jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hiyo yenye nia ya kuhamasiha baa za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli kwenye upande wa huduma inatarajiwa pia kuwafikia wakazi mbalimbali wa mikoa mingine nchini kama;- Arusha, Mbeya, Moshi, Mwanza na Morogoro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: