Bodi ya Ushauri, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wanasikitika kutangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bodi ya TAA, Inj. Lambert W. Ndiwaita kilichoteka tarehe 20/08/2015 katika Hospitali ya Nairobi, Kenya. Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake mjini Bukoba tarehe 25/08/2015.
Mhandisi Lambert Ndiwaita (64) ni mmoja wa wataalamu waliobobea katika masuala ya usafiri wa anga kitaifa na kimataifa, katika kipindi cha uhai wake ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini na nchi nyingine duniadi.
Alianza shughuli zinazohusiana na usafiri wa anga mwaka 19971 alipoajiriwa na iliyokuwa Wizara ya Ujenzi kama Mhandisi Msaidizi na baadaye alipanda hadi kufikia cheo cha Mhandisi Mkuu (Chief Engineer) akishughulikia masuala ya baeabara na viwanja vya ndege. Mwaka 1993 alikwenda kufanya kazi katika Idara ya Usafiri wa Anga nchini Botswana kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Mwaka 1994 aliajiriwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga International Civil Aviation Organization (ICAO) kusimamia masuala ya viwanja vya ndege (Aerodrome & Ground Aids) kwa eneo la Mshariki na kusini mwa Afrika, katika ofisi za ICAO zilizopo jijini Nairobi, Kenya.
Mhandisi Ndiwaita ni msomi aliyehitimu Shahada ya kwanza ya Uhandisi (Bsc Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Mwaka 1978 alihitimu masomo Shahada ya Uzamili (Msc in Civil Engineering) katika Chuo kikuu cha Califonia, Berkley, nchini Marekani akijitikita zaidi katika masuala uhandisi wa ujenzi wa viwanja vya ndege.
Marehemu Lambert Ndiwaita atakumbukwa na wadau wa usafiri wa anga nchini na duniani kwa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta hiyo ambapo kwa hapa nchini akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAA amechangia kufanikisha ujenzi na uboreshaji wa viwanja kadhaa vikiwemo Mwanza, Tabora, Kigoma, Songwe, Mafia, Mpanda, Bukoba na Julius Nyerere (JNIA).
Mungu ailaze roho marehemu mahala pema peponi.
Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu - TAA.
24th AUGUST, 2015



Toa Maoni Yako:
0 comments: