Nilitamani nifanye kipindi na POLE POLE ili nimjibu hoja zake japo hazina mashiko kwenye siasa ni muda sasa tumeanza kuielewa sura ya halisi ya POLEPOLE.

Huyu jamaa kipindi cha Katiba Mpya ndiyo nilimjua baada ya kujinasibisha na uzalendo kwa taifa lakini alipoona CCM inaelemewa akaibuka na kuamua kulitetea CCM amekuwa akimshambulia mgombea wa CDM Mhe. Edward Ngoyayi Lowasa kuwa hafai kuchaguliwa tena akaenda mbali akatuaminisha kuwa eti huyu ndiye aliyefanya mpaka katiba mpya ikakwama.

Nimejaribu kufuatilia hoja zake asilimia mia (100%) hazina mashiko kwa mfano kutuambia kuwa alizuia Katiba Mpya nikutuhadaa Watanzania nani asiyejua msimamo wa CCM juu ya serikali mbili rejea hotuba ya Jakaya Kikwete siku ya ufunguzi wa bunge maalumu la katiba alipotuambia serikali tatu haiwezekani labda awe ameondoka madarakani hii yote ni kuonyesha masilahi ya CCM na serikali mbili yalivyo kitaasisi kuliko MTU.

POLEPOLE ameendelea kutuambia CCM ilimkata Lowasa kwasababu si msafi hapa napo kuna maswali ya kujiuliza Lowassa kajiuzulu 2008 na 2010 alipitishwa na CCC ya ccm kugombea Ubunge wa Monduli sasa kama alikuwa si msafi kwanini walimpitisha ama pia kwanini aliendelea kuwa mtu muhimu kwenye chama maana aliendelea kupewa majukumu kama alivyochaguliwa kuiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya bunge pia kuwa mwenyekiti wa kamati mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki hizi zote kama Lowasa alikuwa hakidhi angeondolewa toka 2008 alipojiuzulu.

POLE POLE anatakiwa kutuambia je? aliwahi kushitakiwa juu ya Richmond iliyobadilishwa na hao anaowatetea na kuiita Symbion Power hakuwai hata kuitwa polisi wala kushikiliwa sasa hizi porojo zako zinatoka wapi? lakini wewe unatuambia kwa maneno tu bila udhibitisho juu ya ufisadi wa Lowasa kuhusu CDM kumuita ni fisadi haikukosea hata kidogo kama ilikosewa inamaana Richmond haikuwepo lakini Lowasa aliwajibika kisiasa na hilo halina ubishi alikuwa na uwezo wa kulikataa azimio kama alivyofanya pinda kwenye Escrow pia katika list Yetu yupo mpaka "mkuu" na mwingine mstaafu na juzi katuita sisi ni wapumbavu na molofa.

Tutamuonesha nguvu ya malofa na wapumbuvu Oktoba 25, 2015 hakuoji wengine walikuwepo kwenye list lakini Lowasa katufungulia njia mkataba ulisainiwa kwa shinikizo la mamlaka ya juu kasema yeye nilitegemea angekuwa kakamatwa ili akadhibitishe mamlaka ya juu ilihusika vipi?.

POLEPOLE angejikita zaidi kiuchambuzi usio na maegemeo usituamishe tuache kusikiliza masuala ya msingi matokeo yake ukatulazimisha kudili vitu ambayo sio masuala yanayopaswa kuzungumzwa kwasasa, nilitegemea utueleze CCM imetekelaza nini juu ya afya, elimu na umasikini umepungua au umeongezeka vipi??? Reli ya kati inayoahidiwa kila uchaguzi unapifika vipi??? shirika letu la ndege ATC lina uhai kiasi gani??? vipi kuhusu mahosipitali Yetu???

POLEPOLE salamu zikufikie popote ulipo, ujue Tanzania ya leo tofauti na ya juzi waloambiwa sio wapiga kura... Leo ndiyo wamejiandikisha tena wamechoka na ahadi zisizotekelezeka.

Wako katika ujenzi wa taifa, Dismas Mwacha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: