Kiwanda cha saraji cha Lafarge kilichopo Mbeya. Kiwanda hiki ni maarufu kwa utengenezaji wa saruji, kokoto na zege.
Wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha Lafarge kilichopo Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja. Lafarge ni mdau mkubwa katika bishara ya Saruji, Kokoto na Zege. 

---
Kampuni mbili zinazoongoza katika sekta ya ujenzi hapa nchini, Lafarge S.A. na Holcim Ltd zimekamilisha muungano wao uliosubiriwa kwa muda mrefu na kuunda kampuni moja itakayo fahamika kwa jina la LafargeHolcim.

Vigezo muhimu vya kukamilisha muungano huo vimeafikiwa hivi karibuni kufuatia ubadilishaji wa umiliki pamoja na kutolewa kwa hisa mpya za Holcim kwenda kwa wanahisa wa Lafarge. 

Wanahisa wa kampuni ya Holcim walipitisha azimio hilo la muungano katika mkutano mkuu uliofanyika Mei 8, 2015.

Wakati wa uzinduzi wa Kampuni hiyo, LafargeHolcim ilizindua pia nembo yake mpya ambayo itatambulisha ushirika baina ya kampuni zote mbili huku ikidhihirisha uongozi na nguvu mpya ya kampuni hiyo. 

Akizungumzia ubia huo, Mwenyekiti msaidizi wa bodi ya wakurugenzi LafargeHolcim Bw. Wolfgang Reitzle, alisema “Tukio hili la leo ni la kihistoria – sio tu kwa kampuni hizi mbili mama, bali kwa sekta nzima ya ujenzi kwa ujumla.  LafargeHolcim ni kampuni yenye sifa za biashara za kipekee, ina sifa ya kuigwa katika sekta ya R&D na huwapa wateja wake bidhaa mbalimbali zenye ubunifu na zenye kuongeza thamani, huduma na ufumbuzi – kuanzia washika dau wadogo hadi makampuni makubwa na miradi migumu.” 

Naye Mwenyekiti msaidizi wa Bodi ya wakurugenzi wa LafargeHolcim, Bruno Lafont, alisema “Kampuni hii mpya imejengwa katika msingi mzuri wa historia ndefu na utamaduni wa Lafarge na Holcim na washirika wake. 

Muungano huu hauwaletei watanzania tu kampuni ya kimataifa, bali pia bidhaa zenye uwezo wa kipekee”.

Hii ni habari njema kwa Tanzania kwani Lafarge ina uwepo mkubwa na ni mbia mkubwa katika kampuni ya Mbeya Cement, ambapo Serikali ya Tanzania na NSSF ni wabia wake pia. 

Akizungumza na wafanyakazi wa Lafarge Tanzania katika hafla ya chakula cha mchana, Ms Catherine Langreney, mkurugenzi mtendaji kwa nchi za Tanzania na Malawi, alisema “Nina Imani muungano huu utawezesha Lafarge Tanzania kuzalisha faida kubwa kwa wabia wake, wakati huo huo kuwa chachu ya ukuaji katika sekta ya Ujenzi na kuleta ufumbuzi mbali mbalimbali katika sekta yenye kubadilika kila siku” 

Bi. Langreney aliongezea kuwa: “Afya na Usalama wa watanzania ndio kiini cha biashara yetu hivyo tupo hapa kushughulikia mahitaji ya wateja wetu na hatimaye kuwa mshirika mzuri wa biashara”

Mwezi April 2014 kampuni hizo mbili zilitangaza nia ya kuungana. 

Baada ya mazungumzo ya kina yaliyokuwa chanya na mamlaka husika kuafikiana, Kampuni hiyo mpya iliweza kupokea vibali vyote husika katika muda uliopangwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: