Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho. Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
---
MSANII maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' amejiunga na chama kipya cha siasa cha ACT Wazalendo. Frank amejiunga na chama hicho leo jijini Dar es Salaam akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika hafla hiyo ya utambulisho kiongozi mwingine ambaye ni Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck pia amejiunga na chama cha ACT Wazalendo na kukabidhiwa kadi za chama hicho.

Akiwakabidhi kadi za ACT-Wazalendo, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa leo Makao Makuu ya ACT alisema wamewapokea wanachama hao wapya kwa mikono miwili na wapo tayari kushirikiana nao ndani ya chama hicho. Alisema kuna idadi kubwa ya vigogo kutoka vyama vingine ambao tayari wameomba kujiunga na chama chao na taratibu zinafanywa kutambulishwa.

"...tendo hili la leo la kuwakaribisha vijana hawa ni mwanzo wa kuwatambulisha wanachama mbalimbali wakiwemo wabunge na viongozi wa vyama waliojiunga nasi baada ya kuvunjwa kwa Bunge. Tayari tunao baadhi ya watu waliokuwa wabunge na wameshajiunga nasi na mchakato wa kuwatambulisha unaendelea katika maeneo mbali mbali nchini," alisema Mtemelwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: