Dr. Chris Mauki aliwahi sema ni ajabu kuona kuna wanandoa wanaishi kama mabachela. Kila stage ina tabia stahiki unatakiwa iwe developed ili kukuwezesha kuishi katika stage husika.
Ukiwa kwenye ndoa ukawa unaishi kama bachela watu wanakushangaa wanasema lakini wewe si umeoa ama olewa?na ukiwa bachela ukijiweka weka kama umeolewa ama umeoa watu wanakushangaa utasikia wanasema siku zote mie najua umeolewa kumbe single?kumbe kuna mkao wa ma single na mkao wa ma couplez mtu yeyote anayeishi.stage sio yake anazaa.tatizo.
Kuna mambo usipoweza kuyafanya ukiwa single huku una uwezo wa kufanya basi tarajia jambo lile lile unaweza usilifanye kabisa ukishakuwa na mwenza. Na kuna mambo ukiwa single utayafanya kwa ustadi na jambo lile lile pengine ukiwa na mwenza unaweza usilifanye kwa ustadi ule ule ama ukashindwa kabisa kufanya na pia kuna mambo mnaweza fanya mkiwa wawili lakini jambo lile lile mnaweza msilifanye tena katika ubora ule ule.
Changamoto ni kwamba katika mambo yote kiroho kimwili kisaikolojia kiuchumi familia yako na jamii inayokuzunguka inakutegemea kukua na sio kurudi nyuma. Ili uweze kutoa lazima uwe umeingiza ndani ya nafsi yako ndani ya account yako pia ndani ya roho yako. Ukiwa na familia itatamani kuwa na muda na wewe,kuwa na furaha na wewe,kuhudumiwa mahitaji yao na wewe wakati huo Boss wako anahitaji muda na wewe jamii inahitaji muda na wewe na nafsi yako pia inahitaji muda na wewe.
Swali la kujiuliza unailisha nini nafsi yako na moyo wako ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo,nini unafanya kuweza kukidhi mahitaji ya familia yako. Kwa Mwanaume kuwa kichwa cha nyumba sio Kunukuu tu maandiko ila KUWAJIBIKA kwa ajili ya ustawi wa watu wa nyumbani kwako. Asiyewajali wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko asiye amini.
Nani kwako ni top 3 na watu wakajua kabisa bila changa wengine namba 1. Simu 2. Hela 3. Familia wengine 1. Pombe 2. Michepuko 3. Kazi wengine 1. Mungu 2. Familia 3. Kazi...
wengine 1. Kuuza Sura 2. Mizinga 3. Kuchat.......Top 3 ya maisha yako inatafsiri sana Hatma ya Maisha yako ya Kesho.



Toa Maoni Yako:
0 comments: