Mpuuzi yeyote hufurahi mno anapomwona mtu analalamika, na mimi nasema Watanzania tulio wengi tunachukua muda mwingi mno kulalamika na si kuweka mipango, Oktoba ni kesho kutwa na tumeshamwona nani mwenzetu na nani mpuuzi, tufanye maamuzi, majitu sahiz yamekomaa na #team badala ya kupigania Nchi, hela zikiisha yalizohongwa ndo utayasikia yanalalamika shemeji katufanya hivi shemeji katufanya vile ujinga mtupu, hivi tumerogwa na nani?
Mkulima unadanganywa na sera dhaifu za kilimo kwanza, kilimo kiko kijijini pembejeo ziko Dar zinafanya nini? Kulima mnalima, masoko hakuna na wala hakuna anayejishughulisha na hilo, mtakufa njaa nyie
Kijana unapelekwa VETA kusomea ufundi, Viwanda hakuna huo ufundi unaupeleka wapi zaidi ya kuanzisha vijiwe vya kutengeneza vibatari, shtuka mtanzania
Hospitali hazina Dawa, unaenda Hospitali ya Wilaya hadi Panadol eti unaelekezwa kanunue duka lilee, hilo Duka la mtu binafsi lilipataje Dawa hospitali ikakosa?
Kila siku majitu mazima yanapiga kelele eti vijana mjiajiri vijana mjiajiri, familia zao Baba, Mama, Mtoto, wote wajumbe wa NEC, saa ngapi watajua kama Mtaji ni tatizo? Hivi unawezaje kujiajiri bila mazingira wezeshi?
Wafanyakazi wengi wanakufa maskini kwa sababu Serikali inawanyonya mpaka kwenye mifupa, mtu mshahara 400,000/= halafu take home 290,000/=, kweli are you serious? Huko mijitu bila aibu inasema tumeongeza mafao ya wastaafu kwa 100% (kutoka 50,000/= hadi 100,000/=) kweli, yani mzee aliyelisotea Taifa lake kwa zaidi ya miaka 30 ya maisha yake leo unaona raha kumpa Mil.1 kwa mwaka is it possible, aibu huwa mmezihifadhi wapi mnapotamka mambo kama haya? Mzee huyu bila shaka hata kiinua mgongo chenyewe alipata Mil.7, leo hii Mbunge mmoja anajinyakulia Mil. 230, halafu eti majitu hata hayashtuki?
Tatizo la watanzania tumeshakubali kutenganishwa, hatuko pamoja tena, ukiona mfanyabiashara anasumbuliwa na miradi isiyoeleweka kama ile ya mashine za EFD basi wewe Mwalimu unaona halikuhusu, unapomwona Mkulima analalamika Pembejeo basi wewe Dereva wa Basi unaona halikuhusu wakati huo huo unasahau kama familia yako inategemea Kilimo, amkeni watanzania, tuzungumze kama Taifa, tunategemeana ktk mahitaji, udogo wa mshara wa Mwalimu una athari ya moja kwa moja kwako mfanyabiashara wa Viazi
Wakati wa kumwondoa asiyefaa ni sasa, kajiandikishe, mwamshe aliyelala mwambie Nchi imeshauzwa, mwambie ukweli kwamba Mwekezaji wa madini anapokuja anapewa miaka 5 ya kufanya kazi bila Kodi huku mzawa akifungua kibanda cha Saluni, hata kabla hajamaliza kukipaka rangi anatakiwa aonane na TRA, mwambie mwaka jana pekee ripoti ya CAG inaonyesha zaidi Bilioni 800 zimepigwa na familia zisizozidi sita, ndo mfumo wa sasa.
Ni wakati wa #TeamTanzania, achaneni na #teammatumboyawatu



Toa Maoni Yako:
0 comments: