Na Mwandishi Wetu

MWANAHABARI Michael Shija Machellah aliyewahi kufanyia kazi Kampuni ya New Habari 2006 Limited inayozalisha Magazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Bingwa na Dimba na baadae Business Times na Majira amejitosa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Udiwani Kata mya Makumbusho jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Machellah alisema ameamua kutia nia ya kuwania kiti hicho baada ya tafakari kwa kina mwenyewe kutoka moyoni akiwa na nia thabiti ya kuleta mabadiliko katika eneo analoishi endapo Chama CHA CCM kitampa ridhaa ya kugombea eneo hilo na kuking’oa Cha cha CUF.

Alisema Machellah yeye ni mzaliwa wa Mwananyamala, Kata ya Makumbusho na anaishi Kata hiyo jijini Dar es Salaam hivyo anakilasababu ya uzalendo wa kutia nia kwa maana halisi ya kutaka mabadilijko katika Kata yake kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.

Machellah alizaliwa tarehe 19/08/1975 Katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar ews Saalam, Alipata elimu ya Msingi Kijijini kwa Wazazi wake Mwime Kahama Mkoani Shinyanga, Alipata Elimu ya Secondari katika Seminari ya Mt.Joseph Ujiji Mkoani Kigoma na ana Diploma ya taaluma ya Uandishi wa Habari ambayo ajiipata jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Dar es Salaam School of Journalism(DSJ).

Machellah kwa sasa ni Mwajiliwa katika Kampuni ya Integrated Communications Limited kama Afisa habari katika kitengo cha Mawasiliano na mahusiano (PR) cha moja ya vitengo vya Kampuni hiyo. 

Wito kwa wakazi wa Kata ya Makumbusho kwa mwaka huu wa uchaguzi wasifanye kosa walilolifanya awamu iliyopita jiandae vyema kukirudisha Chama cha Mapinduzi Madarakani katika Kata yako na zaidi Mchague Michael Machellah(NGOSHA) kwa maendeleo ya Kata yako ya Makumbusho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: