Nyumbani na Diaspora!

Ni kipindi kipya cha saa nzima chenye kuhusiana na Watanzania wa nyumbani na walio nje ya mipaka yetu. Ni kipindi daraja kitakachowaunganisha Watanzania katika kubaini fursa mbalimbali za kuinuka kimaendeleo, kwa mtu mmoja mmoja, jumuiya na hatimaye taifa. Ni kipindi kitakachoongozwa na mchambuzi na mmoja wa wanahabari nguli hapa nchini. Si mwingine ni Maggid Mjengwa. Jiunge nae kufuatilia mahojiano motomoto na watu wa kada mbalimbali kwenye masuala ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Ni kila siku ya Ijumaa saa 4 usiku na marudio Jumapili saa kumi jioni, hapa hapa TBC 1, ukweli na uhakika!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: