Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula akizungumza katika kikao chake cha kwanza na Watumishi wote wa Wizara tangu alipoteuliwa na Rais hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mkutano huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Juni, 2015. Pamoja na mambo mengine Balozi Mulamula aliwahimiza Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje kufanya kazi kwa bidii, kuwa na utii, nidhamu pamoja na unyenyekevu ili kufikia malengo katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.
Home
Unlabelled
KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AFANYA MKUTANO NA WAFANYAKAZI WOTE WIZARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments: