Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (mwenye suti ya bluu) Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb) wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Comoro Mhe. Ikililou Dhoinine (mwenye mavazi meupe) pamoja na viongozi, wafanyabiashara na wadau kutoka Sekta Binafsi baada ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya nchi ya Comoro na Tanzania lilioanza tarehe 23 Aprili, 2015.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza, akitoa hotuba yake baada ya ufunguzi wa kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya nchi ya Comoro na Tanzania kwa wadau na wafanyabiashara kutoka Tanzania (hawapo pichani). Kongamano hilo limeanza tarehe 23 Aprili, 2015 likiwa na lengo la kufungua fursa mpya za biashara na uwekezaji nchini Tanzania na Comoro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: