Rais wa Heshima wa Timu ya Barcelona Kocha Johan Cruyff, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar alipofika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Kikosi cha Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakitokea Arusha, wakiwa Zanzibar kwa Mualiko wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kutembelea Zanzibar kujionea Vivutio vya Utalii na kujionea Vipaji vya Wachezaji Vijana wanaocheza katika timu mbalimbali za Watoto.
Waandishi wa habari za michezo Zanzibar wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa kuipokea Timu ya Wachezaji wa Wazamani wa Timu ya Barcelona
Kikundi cha ngoma wakitowa burudani wakati wa ujio wa Wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona Zanzibar. kwa ziara ya siku moja Zanzibar. kwa mualiko wa Rais wa Zanzibar Dk Shein.
Viongozi wa Vyama vya Mpira Zanzibar wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wakiipokea timu ya Wachezaji wa zamani wa Barcelona walipowasili Zanzibar.
Ndege ya Serekali ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na Wachezaji wa Mastar wa Zamani wa Barcelona wakiwasili Zanzibar kwa ziara ya siku moja kwa mualiko wa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohemed Shein, na kujionea Vipaji vya Wachezaji wa timu za Watoto katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Bi Shery Khamis akisalimiana na mchezaji nyota wa timu ya wachezaji wa zamani wa Barcelona Kulvert alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya siku moja Zanzibar.
Wachezaji Nyota wa Timu ya Barcelona wakisalimiana na Viongozi wa Vyama vya Michezo Zanzibar baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya siku moja kwa mualiko wa Rais wa Zanzibar Dk Shein.
---
Na Mwandishi wetu
Mashabiki wa soka kesho watawashuhudia wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert, Gaizka Mendieta , Anderson De Soursa “deco” Francesco Coco na Luis Garcia wakionyeshana kazi na wakali wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hii itakuwa mara ya pili kwa watanzania kushuhudia mastaa hao wa zamani wakikipiga kwenye uwanja huo baada ya wale wa Real Madrid waliokuwa chini ya Luis Figo, Christian Karembeu na Fabio Cannavaro wakicheza kwenye uwanja huo kwa mara ya kwanza na kushuhudiwa na Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikosi cha FC Barcelona kimesheheni wachezaji nyota wengi mbali ya Kluivert na wenzake ambao kwa mashabiki wa soka ni majina maarufu. Wachezaji wengine ambao wanatarajia kushuka leo uwanjani chini ya kocha maarufu, Johan Cruyff mi pamoja na makipa nyota, Jesus Mariano Angoy Gil na Robert Oscar Bonano.
Wengini ni Sergi Barjuan Esclusa, Albert Toams Sobrepera, Luis Milla Aspas, Lluis Carrreras Ferrer, Miguel Angel Nadal Homar, Ion Andoni Goikoetxea Lasa, Oscar Arpon Ochoa, Santiago Ezquerro Marin, Javier Villena Mulero, Magin Civantos Martinez, Mateo Segura Capellades na Simao Sabrosa.
Kocha wa timu hiyo, Cruyff alisema kuwa wamekuja kuonyesha vipaji vyao vya zamani vilivyotukuka na hakuna wa kuwazuia kushinda katika mechi ya leo. Alisema kuwa wachezaji wake wegi japo wameacha soka, bado wanajihusisha kwa kufundisha na wengine kufanya mazoezi kwa ajili ya timu yao “FC Barcelona Legends”.
“Tupo vizuri, tumejiandaa kwa ajili ya kuweka historia, tunajua wenyeji wataleta upinzani, lakini sisi ndiyo tutakuwa washindi,” alisema Cruyff kwa kifupi.


Toa Maoni Yako:
0 comments: