Naomba nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa TCRA kupitia CloundsFM kuhusu Sikika na Mswada wa ‪#‎CyberCrimeBill‬.


Sikika haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na leo maafisa wa TCRA.


Sikika haikutoa maoni kuhusu Mswada wa miamala ya kielektoniki kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na pia leo maafisa wa TCRA.


Sikika ilituma maoni ya pamoja ya wadau kwa niaba ya wadau kuhusu #CyberCrimeBill kwa njia ya email kwa Mkiti Kamati Mh Peter Serukamba.


Maoni hayo hayakutumika kuboresha #CyberCrimeBill bali kuongeza tu orodha ya wadau wanaoda iliwa "kushiriki" kwa lengo la kuonesha kuridhia.


Kwa kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba ‪#‎CiberCrimeBill‬ iliyopitishwa ina mapungufu mengi, Sikika na wadau bado wanaipinga.

Mwisho tunaomba jina la Sikika lisiendelee kutumika kuhalalisha upitishwaji wa sheria hii.

Irenei Kiria
Mkurugenzi wa Sikika
4 Aprili 2015.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: