Leo nimeona tupeane mipaka ya hawa dada wanaosaidia majumbani. Sasa vema tukajua mipaka yao ndani ya nyumba.

KWANZA: Asiguse kabisa mlango wa kuingia chumbani kwa mabosi wake... hapa nazungumzia suala la kutoingia chumbani kama ambapo baadhi wamekuwa wakiwaruhusu mahausigeli kuingia na kufanya usafi... jambo ambalo kimaadili halikubaliki. 
*Msichana wa kazi afanye usafi kote lakini chumbani asiruhusiwe.

PILI: Hausigeli asiwe na mawasiliano ya karibu na baba mwenye nyumba... sasa hivi zipo simu za mkononi zinatumika kurahisisha mawasiliano... lakini hausigeli hata siku moja asipewe mwanya wa kumpigia simu baba mwenye nyumba au kumtumia sms. *Baadhi wamekuwa wakiona si jambo baya matokeo yake inapotokea msichana wa kazi ni mcharuko na baba mwenye nyumba naye hajatulia... wawili hao wanaweza kufungua ukurasa wa mapenzi.

TATU: Hausigeli asihusike katika suala la kufua nguo za ndani za mume... Hapa namaanisha soksi,boksa, singilendi na nyinginezo jukumu libaki kuwa la mama mwenye nyumba.

NNE: Hausigeli asiruhusiwe kukaa sebuleni kama baba mwenye nyumba yupo. *Sasa jifanye unajua kuishi kizungu mumeo aangalie tamthiliya na hausigeli... hii si sawa kabisa.

TANO: Wakati hausigeli anakwenda bafuni kuoga kwanza asiwe amevaa nguo nyepesi kama vile kanga moja ahakikishe haonani na baba mwenye nyumba.

SITA: Hausigeli asipewe nafasi kumuandalia kitu chochote mume... kwa mfano chakula, maji ya kuoga, nguo za kuvaa na vinginevyo. 
*Hii ni kazi ya mama mwenye nyumba lakini utashangaa baadhi ya kina mama wanajibweteka naenga matokeo yake wanajikuta wameporwa waume zao.

SABA: Hausigeli asitoke out na baba mwenye nyumba. 
*Hapo ndiyo mwanzo wa kujenga mazoea... acheni kujifanya wazungu eti hausigeli anampeleka mtoto beach na baba mwenye nyumba...

NANE: Hausigeli hata kama ana shida vipi... asipewe nafasi ya kumweleza shida zake nwenye nyumba... hata mshahara inashauriwa mama mwenye nyumba ndiye wa kumkabidhi na si vinginevyo. 
*Hakikisha hakuna mwanya wa mumeo kumnunulia vijizawadi msichana wa kazi kwani madhara yake ni kuingia kwenye mapenzi.

TISA: Hausigeli asimzoee mumeo kiasi cha kuona ni sawa kuzungumza naye wakati wowote kutaniana taniana na mumeo akomeee.

TUZITUNZE NDOA ZETU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: