Kamanda wa uvccm wilaya ya Iringa mjini Frederick Mwakalebela akiwahutubia wananchi ktk uwanja wa mwembetogwa ktk mkutano ulioandaliwa na uvccm Iringa mjini

Wananchi Iringa mjini wakiwa ktk mkutano wa uvccm Iringa mjini

Kada  wa CCM Bw Ahmed Mbata  mwenye miwani akimzuia  kijana wa CCM kuendelea  kumthibiti kada wa Chadema  aliyeanguka chini baada ya  kupigwa  kwa  tuhuma za  kutaka  kuvuruga mkutano wa UVCCM
Vijana  wa CCM  wakisogea  kumshambulia  kijana aliyetaka  kuvuruga mkutano  wao
Wananchi  wakimtazama  kijana  wa Chadema aliyetaka  kuvuruga  mkutano wa CCM
Wananchi  wakitazama  tukio  hilo.
Askari polisi akizuia  vurugu  hivyo
Mwakalebela  kushoto  akiwa na katibu wa UVCCM  Iringa

Na MatukiodaimaBlog

KAMANDA  wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Iringa mjini Frederick Mwakalebela atuma   salam kwa upinzani  jimbo la Iringa mjini  kuwa mwisho wao kuongoza jimbo hilo ni oktoba  mwaka huu hivyo wananchi wajiandae kwa sherehe za kulipokea jimbo.

Akizungumza leo   katika mkutano wa uvccm Iringa mjini uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa.

Alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akikodi majeshi (wanasiasa wenzake) nje ya Iringa mjini ili kusaidia mashambulizi baada ya  kuona  hali ya upepo kwakwe  si nzuri.

"Naomba kuwahakikishieni kuwa jimbo hili tulikosea mwaka 2010 ila kwa mwaka huu haturudii kosa lazima jimbo lirudi CCM"

Hivyo alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa lazima Chadema wajipange kukabidhi jimbo hilo kwa Ccm na kuwa maandalizi ya kupokea yamekwisha fanyika.

Akielezea kuhusu umuhimu wa vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura alisema ili Ccm uweze kushinda kuanzia udiwani ,ubunge na Urais ni lazima wakajitokeza kujiandikisha ktk daftari hilo .

Kwani alisema hakuna ushindi bila ya vijana kujitokeza kujiandikisha na kuwa iwapo kila mmoja atajiandikisha ushindi wa CCM upo wazi .


Kwa upande  wake katibu wa CCM mkoa  wa  Iringa  Hassan Mtenga  akihutubia 
wananchi hao  alisema  kuwa   mbunge msigwa  anapaswa  kujiandaa kisaikolojia  kwani CCM imejipanga  vema  kuona  jimbo  hilo  linarudi  mikononi mwa CCM kwa  mwaka  huu .


Alisema  kuwa  jimbo hilo CCM kililianzimisha kwa Chadema hivyo muda wao wa  kuendelea  kulikalia umepitwa  kutokana na  mbunge kushindwa  kuwatumikia  vema wananchi wa  jimbo  hilo wakiwemo  vijana ambao  waliahidiwa ajira  ila hadi leo vijana Iringa mjini  wamegeuka omba omba kutokana na  kutokuwa na ajira.

Hivyo  alisema  mbali ya  mbunge  wa  sasa muda  wake  kumalizika bado anapaswa  kuwaeleza  wananchi wa  jimbo la Iringa  mjini matumizi ya  fedha za mfuko wa jimbo ambazo amekuwa akizipata  zimefanya kazi gani katika   jimbo  hilo lasivyo CCM itakuja na orodha kamili ya ahadi  zake na  kiwango halisi  cha   fedha za mfuko wa  jimbo .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: