Nilipofika ndani nikapanda ngazi haraka haraka akanifuata, wakati huo mie napanda ngazi moja moja yeye mbili mbili kabla sijafika hata mlangoni akanivuta akanishusha chini akasema leo nakuuwa... siwezi penda mwanamke nikampa kila kitu anachotaka kisha anisaliti alinipiga sana pale chini... salama yangu ni kijana wa getini kuja kuniokoa maana nilipiga kelele kama nimekalia moto.

Hakuongea aliponipiga nikaokolewa akaenda kwenye wine space akakaa huko akaanza kunywa wine... huku analia sana... nikaingia chumbani nikaanza kulia asubuhi kufika nikamkuta kalala pale pale juu ya meza ya wine, sikumsemesha kitu... nilivaa nikaondoka kwenda kazini... sijui aliamka saa ngapi?.. ila mida ya mchana akanipigia simu sikupokea... akapiga nikakata akatuma meseji pokea simu mke wangu wala sikupokea.

Niliporudi jioni kaka wa getini akasema shemeji nae kaondoka sasa hivi toka asubuhi ameamka alikuwa analia tu. Kaja rafiki yake wameondoka... sikujibu kitu nikafika.... kidogo ikaingia meseji kwamba nimfate Samaki Samaki kule Mliman City ...nikamjibu siji ... sijakaa sawa akamtuma mtu anifate nikaenda kufika akaniomba radhi sana mbele ya rafiki yake kwa kunipiga... Yeye mwenyewe anajutia kwanini alinipiga aliomba radhi sana nilimshangaaa kukuta anakunywa pombe wakati alikuwa hanywi nikamuuliza Franco... when did you start this???... akajibu Yesterday... and it's becouse of you... basi aliomba radhi na wenzie wakanisihi nimsamehe tukarudi home... that day ilikuwa full malavidavi ... lakini upande wangu niseme kweli yule kijana Kelvin aliniroga jamani... wakati nipo kwenye malavidavi na mume wangu huku namkumbuka Kelvin.

Za mwizi zilifika ambazo hadi leo najiuliza sijui alijuaje hoteli niliyokuwa nimeenda kulala na Kelvin... nawaza hadi leo nakaribia miaka miwili toka nimeachika sijui alijuaje Franco.

Ilikuwa siku ya Jumamosi Kelvin akaniambia kuwa ameninunulia kiwanja Mkuranga niende akanikabidhi... hakusema kama nitalala huko sikujipanga kuaga chochote ... nikamwambia Franco naenda kwenye Chama tuna kikaon huko Mbagala akasema sawa nenda... nikaondoka kufika huko tukakaa bar moja hivi tukala... akaenda kunionyesha hicho kiwanja nikakitazama tulipomaliza kukiona akasema twende kwenye kituo chake kimoja cha mafuta mbele ya Mkuranga.

Wakati huo ilikuwa saa 12 jioni nikamwambia si unajua natakiwa kurudi home akasema ndiyo nafahamu hatukai sana... tulipaki gari yangu nyumbani kwake Kawe tukaondoka na gari yake. I was comfortable kwa vile gari ilikuwa ni full tinted (ukisema uchungulie ndan unajiona sura yako unavyochungulia ndani huoni kitu).

Kufika huko tukatembelea kituo chake nikapaona... Kelvin alikuwa hajaoa kabisa hivyo nilikuwa fee kwake... akaniintroduce kwa wafanyakazi wake kama mkewe mtarajiwa... bad enough nilikuwa nikikutana na Kelvin tu ananiambia toa mapete yako.. na kuna siku alitaka kuzitupa alisema hazipendi ikawa ugomvi basi nikawa nazivua.

Baada ya hapo akaniambia anafeel joto nimsindikize kupaga hoteli moja hivi na akasema hawezi niacha bila kumpa malavidavi nami kuonyesha ushirikiano wa kiwanja kile nikaenda ila kwa makubaliano tukimaliza tunarudi nyumbani ... siku nzima sikuwa nimeongea na wale mabest zangu hata mmoja... tukaenda hotelini huko huko Mkuranga.

Tukiwa hotelini pale baada ya malavidavi akaniambia leo huondoki... simu hii hapa mpigie mmeo sema unavyosema leo tunalala wote nikalia sana akanipokonya funguo za mlangoni... akasema siku nikisikia mme wako kafa nitafurahi sana... hana hadhi ya kumiliki mtoto mzuri kama wewe.

Nililia aniruhusu kuondoka akagoma... basi mida ya saa mbili simu ikaita kucheki ni mme wangu... nikafungua madirisha ili mwangwi utoke nikapokea nikamwambia nimepitia msibani kuna rafiki yangu kafiwa ... akachekaaaaa akasema okay! kwahiyo hurudi? nikasema naweza kuchelewa sana.. akasema haya mke wangu. Nakupenda nikamwambia nakupenda pia. Akakata simu.. hapo nilikuwa na hofu sana.

Nikiwa hapo tulikuwa tumeagiza kuku wa kuchoma nje. Nikasema hatuendi kula nje walete chumbani... basi nilikaa ndani kama saaa moja baada ya kuongea na Franco akapiga tena akasema nipo hapa ulipo naomba nikuone mara moja... Nikashtuka akasema tena unakuja au Mimi nije?... sauti ile ilikuwa kama MTU analia... pembeni nasikia MTU anamwambia Franco utaharibu sasa... nikakata simu.

Nikamuuliza Klevin,  Franco anasema yupo hapa nilipo kuna MTU yeyote ulimwambia tutakuwa hapa leo? Klelvin akajibu huyo mumeo bwege ni muongo anakutishia tu... mie sikumwambia MTU ila niliongea na Rachel asubuhi nikamwambia leo  nakuja kukupa KIWANJA ila sikusema nitakuja hapa.

Simu ikaita tena nikapokea akasema Mke WANGU. Nipo nje... unakuja au nije? Ila sauti yake kama anabana kilio... nikakata simu bila kujibu... Jamani sitakaa kusahau Siku hii huwa nalia sana hapa pia nalia nimekumbuka mbali.

Ghafla simu ya chumban kwetu ikaita... wote tukaogopa kupokea... kidogo mlango wa chumbani ukagongwa... Kelvin akauliza nani? Wakati huo mimi niko hoi jasho linanitoka... mwili unaishiwa nguvu... nikaomba nikasema Mungu wa uzima nitetee kwenye hili naahidi nikitoka salama sitakutenda dhambi tena... nikasahau kama Mungu hasikii maombi ya mwenye dhambi.

Kama mnakumbuka nilikuwa kwenye purukushani za kutaka kumkimbia Kelvin tulipofika... moyo haukuwa na amani kabisa Siku hiyo kwahiyo Kelvin aliuchukua ufunguo ili nisitoroke akawa nao mlangoni kukabaki hakuna kitu chochote cha kuzuia ufunguo mwingine kupita... tukasikia sauti ya muhudumu ikisema Mimi muhudumu fungua mlango.

Kelvin akamfokea... kwanini unasumbua wateja???.. Hii ni sheria ya wapi?? muhudumu kumwamulisha mteja afungue mlango???... hakujibiwa... nikasikia nyayo zikitembea kama zinaondoka vile moyo ukarelax.

Baada ya dakika tano tu nikasikia mlango unafunguliwa ndio nikaju kumbe na hoteli huwa wana funguo mbili mbili na spare... oh! kikubwa zaidi inaniuma mazingira niliyokutwa nayo... Kila nikikumbuka roho inaniuma... I'm crying always.

Nilikutwa nikiwa uchi kabisa nimekaa kwenye kona ya kitanda nimeshikiria MTO... Kelvin akiwa uchi kabisa ameganda kona ya kitanda hajui afanye nini akashika simu...moja haikai wala mbili haikai... anaacha anainuka, anakaaa anaangalia pa kukimbilia... mwisho akasema niingie uvungu wa kitanda... rum tulochukua INA vitanda vya box vile vikubwa sana havina uvungu akatoa godoro ili niingie kupotia chaga za kitanda... ndipo mlango ulipofunguliwa nikiwa nimesimama natafuta pa kuitetea ndoa yangu.

Endelea kufuatilia sehemu ya tano bila kukosa ya sita ambayo itakuwa ya mwisho...
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: