4
Kitengo wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo tayari kwa mashindano ya NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 yanayofanyika kesho February 28 kuanzaia saa 7:00 asubuhi kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Mpaka sasa wachezaji 60 wameshathibitisha kushiriki katika mashindano hayo na wachezaji wengine wanaendelea kujisajiri ili kushiriki katika michezo hiyo ya Gofu, Kapteni Japhet Masai ametoa mwito kwa wachezaji mbalimbali kuendelea kujisajiri na amesema wanatarajia zaidi ya wachezaji 120 watashiriki katika mashindano hayo.

Shindano la NIC Corporate Golf Chalennge linaandaliwa na shirika la bima la taifa NIC na linafanyika kila mwaka kuanzia tangu lilipoanzishwa mwaka 2013 na linashirikisha wachezaji wa rika zote na jinsia zote NIC imeandaa zawadi mbalimbali kwa washindi, ambapo mshindi wa kwanza atapata jiko kubwa la umeme. Pia wshindi wengine watapata zawadi mbalimbali zilizotayarishwa kwa ajili yao ambazo ni meza kubwa ya ofisini, mikoba ya akina mama, mabegi ya wanafunzi, Feni , Friji, Microwave na zawadi nyingine nyingi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 5
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa ya jiko kubwa la umeme Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo 6
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta na Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo wakipiga picha pamoja na zawadi hizo. 7
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta akipiga picha mara baada ya kukabidhi zawadi hizo kwenye viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: