Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba  
akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu, wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), kwa ajili kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamari, katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Buguruni Viziwi jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na (kulia) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abubakar Rakesh na mnufaika wa kibanda hicho, Hebron Mwansele (kwenye baiskeli).Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwatunza pesa wanamuziki ya walemavu ya Bendi ya Tunawajali, iliyokuwaikitumbuiza katika hafla hiyo.
 Sehemu wa wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), wakiwa katika hafla hiyo.
 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikagua kioski baada ya kukabidhi.
---
Katika kuendeleza shughuli zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu yenye lengo la kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali.

Sambambal na hilo Airtel pia imewapatia mtaji wa kuanzisha biashara ili  kuwawezesha watakao nufaika na vibanda hivyo kuwa mawakala wa huduma ya Airtel money na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Saalam.

Akiongea wakati wa hafla ya makabidhiano, Naibu Waziri wa mawasiliano Mh. Januari Makamba alisema” tunapenda kuwashukuru  Airtel kwa kutanua wigo na kutoa msaada kwa watu wenye ulemavu ili  kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. Serikali yetu iko makini katika kuhakikisha kila mtanzania anapata haki sawa bila kubagua makundi natoa  fulsa sawa katika maeneo mbalimbali.

Sisi kama Serikali tunaamini msaada mliopokea leo utakuwa chachu ya kuleta maendeleo ya kiuchumi na nyenzo kwa wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu kujikwamu na tatizo la kiuchumi unaowakumba makundi mengi kama haya katika jamii”.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: