Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi katika Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo hayo uliofanyika leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua rasmi Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, walipoingia katika chumba maalum cha mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo wakati wa uzinduzi wa Majengo ya Taasisi hiyo ya Mafunzo uliofanyika leo.
Mafunzo kwa Vitendo yakiendelea katika Taasisi hiyo,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la viwanja vya Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments: