Bi  Sarah Mungai akiwa na mmoja kati ya  watoto yatima wa kituo cha DBL mkimbizi Iringa
Bi  sarah Mungai akiwa na Mtoto  aliyetupwa na  mama  yake  mzazi ambae anautindia  wa  ubongo  mara  baada ya  kumzaa na sasa anaendelea vema baada ya  kuokolewa maisha yake  na kituo cha DBL Iringa
Mkurugenzi wa kituo  cha DBL Neema Mpeli  kulia akiwa na sarah Mungai
Mkurugenzi mtendaji wa DBL mchungaji Mpeli  Mwaisumbi akimkaribisha  Mungai na mkewe
Baadhi ya  watoto  kituoni hapo
Mchungaji Mpeli  akieleza jinsi ambavyo Mungai alivyokuwa msaada  kituoni hapo
Bi.Sarah Mungai  akisoma  risala ya familia
Mchuungaji Mpeli  akiwashukuru wadau
Watoto yatima  wakifurahia msaada   huo
wageni  mbali mbali  waliofika katika  hafla   hiyo
Sarah Mungai na Mumewe  Geofrey wakitoa taarifa  yao fupi
Mmoja wa watoto yatima  akishukuru
Geofrey na mkewe  wakiwaongoza  yatima  kupata chakula
Mtoto aliyetupwa
Dr Gabone  akishiriki  chakula
Mungai akimlisha chakula  yatima 
kawaida  yake  kwa  kila mwaka katika msimu  wa  sikukuu ya Krismas na mwaka  mpya  kufika katika  kituo hicho na  kuwapa msaada  watoto  hao ili nao  kuungana na  watoto  wenye  wazazi  wao kufurahia sikukuu hizo.

kuendelea  kutembelea  vituo  vya yatima kila mwaka  kwa  ajili  ya kuwasaidia misaada  mbali mbali.
 Na matukiodaimablog

MKANDARASI Geofrey  Mungai  ametoa  msaada  wa  nguo za sikukuu na chakula vyote  vikiwa na  thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2  wa kituo cha  watoto yatima cha  Daily Bread Life Tanzania  (DBL) kwa ajili ya  kusherekea sikukuu ya krismass na mwaka mpya.
Mungai alitoa  msaada huo jana  kwa  uongozi  wa  kituo hicho pamoja na kuwaandalia chakula  cha pamoja   watoto  zaidi   39  na  wananchi mbali mbali wa mji  wa Iringa kama njia ya  kuwahamasisha  kusaidia yatima.

Hata hivyo  alisema  kuwa jamii ya  mkoa  wa Iringa na  watanzania  kwa ujumla wanapaswa  kubadilika kwa  kuelekeza  michango  yao  kwa  watoto yatima ambao baada ya  kupoteza  wazazi  wao  faraja ya  pekee wanaisubiri  kutoka kwa  jamii inayowazunguka.

Aidha alisema  kuwa  yeye  kama mmoja kati  ya wananchi wa Iringa wenye mapenzi mema na watoto yatima hivyo kuwaomba wananchi wengine   kuweka  mpango wa  Alisema kuwa  upo uwezekano mkubwa wa  watoto  hao yatima  kuendelea kusaidia  iwapo watanzania na wadau  mbali mbali   kuwekeza kwa  watoto hao.

Kwa upande  wake  mkurugenzi mtendaji  wa  kituo  hicho  mchungaji Mpeli Mwaisumbi mbali ya  kumpongeza  Mungai kwa  kuendelea  kusaidia  watoto hao  bado wadau  mbali mbali  wameendelea kujitolea kusaidia  kituo hicho .

"watoto  hao wanalilewa  vema na  wapo ambao  wanasoma shule  mbali mbali   na  vyuo  vikuu baada ya kusaidiwa na  wadau"

 Alisema kuwa  kituo  hicho kinafanya kazi  chini  ya  shirika  lisilo la kiserikali  ya Daily Bread  Life  Tanzania lililosajiliwa  kwa  usajili 12903 chini ya  wizara ya mambo ya ndani ya  nchi pia   kituo kimesajiliwa na ustawi  wa jamii kwa  kupewa usajili wa makao  ya watoto namba 00049995.

Hata hivyo  alisema  kuwa  kituo  kilianza  kupokea  watoto  14 mwaka  2004 na  sasa  kuna  watoto 37 waliopo  kituoni  hapo  na  kuwa  toka  kituo kianzishwe  jumla  ya  watoto 51 wamelelewa  hapo.

Alisema kutokana na misaada wa  wadau mbali mbali kituo kimeendelea  kupata  mafanikio makubwa kama  kuwa na  shamba, basi  moja, mradi  wa cherehani pia  tayari   shule  ya  sekondari ya DBL imejengwa na imeanza  kupokea wanafunzi toka mwaka huu  shule  iliyopo  umbali  wa kilomita 6  kutoka mjini Iringa kwa  lengo kuwawezesha  watoto  na wengine  watyakaofaulu na kukosa nafasi  kupata  elimu ya  sekondari.

Pia alisema changamoto  kubwa katika uendeshaji wa  kituo hicho ni michango mingi katika shule za msingi ambako  watoto  hao  wanasoma ,kukosa  ruzuku toka  serikalini na  changamoto  nyingine  nyingi.

Mchungaji Mpeli  aliwaomba  watanzania  na  wadau mbali mbali pale  walipo iwapo  wanahitaji kusaidia  kituo hicho  kutuma  michango  yao kupitia akaunti namba Benk ya Exim ni 5435526007  Daily Bread  Life Childreans home, ama  kwa njia ya M-PESA  0754362536

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: