Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar
Zaidi ya Million 130 zinahitajika ili kuchangia juhudi za serikali katika kutokomeza saratani ya matiti nchini.

Hayo amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Ocean Road, Dkt Diwani Msemo wakati wakuitangaza siku ya matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi wa matibabu ya saratani ya matiti jijini Dar es Salaam.

Dkt Msemo amesema kwamba wagonjwa wa saratani ya matiti wapya million1.4 wanagundulika kila mwaka duniani kote tofauti na wagonjwa wasaratani ya shingo ya kizazi ambao ni laki tano kwa mwaka.

Aidha Dkt Msemo amewaweka sawa wananchi kuhusiana na suala zima la matibabu ya saratani kwa kusema kwamba saratani inataibika hivyo ni vyema mtu akijua ana ugonjwa huu kuwahi hospital mapema na kupata matibabu sahihi.

Mwezi wa kumi ni mwezi mahususi ambao umetengwa na jumuiya ya kimataifa kuhamasisha uelewa kwa jamii juu ya saratani ya matiti Matembezi hayo ya natarajiwa tarehe 12 mwezi huu na Waziri wa afya na Ustawi wa jamii anataraji wa kuongoza mtembezi hayo yatakayoanza na kumalizikia Kunduchi.

Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “KWA MOYO NA MATARAJIO TUNAWEZA KUWA NA TANZANIA HURU ISIYO NA SARATANI YA MATITI”.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: