Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akiwa na ujumbe kutoka mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Kuwait wakisubiri kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya kuanzisha mradi wa maji katika Wilaya ya Same naMwanga. Aliye kulia kwake ni Bw. Abdulwahab A. Al- Bader ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akitia saini makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kulia kwake Bw. Abdulwahab A. Al- Bader ambayeni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Kuwait. Waliosimama nyuma ni Bi. Suzan Mkapa, Mkurugenzi wa sheria kutoka Wizara ya Fedha na wengine ni wataalam kutoka Kuwait.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile na Bw. Abdulwahab A. Al- Bader ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Kuwait wakibadilishana mikataba hiyo baada ya kutiliana saini.
Wajumbe kutoka Tanzania na Kuwait wakishangilia kwa furaha baada kusainiwa kwa mkataba wa kuanzisha mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga.
Picha zote na Ingiahedi Mduma - Wizara ya Fedha tukiwa Washington DC.
Toa Maoni Yako:
0 comments: