Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Smile Communication (Smile) Bi. Linda Chiza (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampeni ya SmileON ambayo itawawezesha wateja kuendelea kuwa hewani mtandaoni pale kifurushi cha intaneti kinapokwisha. Kushoto ni Head of Operational Efficiency and Compliance Bw. Athumani Nzowa na Mkurugenzi wa Mauzo wa Smile Edgar Mapunde.



Kampuni ya Smile Communications (Smile), imekuja na uvumbuzi mwingine wa huduma yao ya mtandao wa 4G wenye kasi zaidi, imezindua huduma mpya yenye lengo la kuimarisha na kuwawezesha wateja wao kuendelea kuwapata huduma ya intaneti pindi kifurushi cha intaneti kinapoisha kabla ya muda.


Ikijulikana kama ‘SmileON’, huduma hii ni ongezeko la thamini ya bidhaa mbalimbali za Smile 4G inayoruhusu wateja kufurahia huduma yakuaminika ya intaneti yenye kasi kubwa kwa watumiaji kujiunga kwenye kifurushi ya 5GB au kikubwa zaidi na kwa wale wanaonunua huduma ya intaneti majumbani (Smile@home), kifurusha cha usiku (Night) na vifurushi vya wikiendi. Wateja hao wataweza kuendelea kupata huduma ya barua pepe, kuperuzi kwenye mtandao, huduma ya Skype, Wikipedia, huduma za kibenki mtandaoni na mitandao ya kijamii kwa spidi yenye kasi kubwa, hata baada ya kifurushi kuisha mpaka watapoweza kuongeza hela na kutumia huduma kamili ya intaneti.
Baadhi ya maofisa wa Smile wakiwa na furaha huku wameshikili vipeperushi vinavyoonesha kuwezesha wateja kuendelea kuwa hewani mtandaoni pale kifurushi cha intanet kinapoisha.

“Huduma hii ni ya kwanza kwa Tanzania. Kampuni ya Smile inaongoza nchini kwa kuwa na kasi kubwa ya mtandao, ubora, urahisi na zaidi tumewasikiliza wateja wetu kwa kutatua kusikiliza mahitaji yao” aliosema Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Smile Communications, Fiona McGloin.
“Bidhaa mpya ya SmileON inawezesha wateja kuendelea kutumia huduma za intaneti kila siku mpaka watakapo ongeza salio”

Bi. McGloin aliongeza kwa kusema kwamba lengo ni kuruhusu wateja wa Smile kuendelea kutumia huduma ya mtandao mpaka watakapoweza kuongeza salio na kuweza kupata huduma kamili kama kuangalia video na kuweza kuhamisha makabrasha makubwa. Anazidi kupongeza uamuzi huu wa Smile kuleta mawazo mapya na njia mbalimbali za kuwapa wateja wanachohitaji ambacho ni intaneti ya haraka zaidi na SmileON inategemewa kusaidia kuongeza ufanisi wa biashara na matumizi ya nyumbani.
Aliahidi kuwa mtandao wa 4G LTE kutoka Smile, ambao tayari sasa uko Dar es Salaam na Arusha utatambulisha bidhaa mpya mbali mbali na za kibunifu zaidi kadri mtandao wa Smile unavyopanuka kuhakikisha watanzania zaidi wanafaidika kupitia huduma ya intaneti yenye kasi zaidi.

Katika mwezi wa Agosti, Smile imewapa wateja fursa yakuchagua spidi ya intaneti wanayoitaka kuwasaidia kusimamia matumizi yao ya intaneti. Kwenye akaunti binafsi ya mteja ya MySmile, mteja anaweza kuchagua spidi ya intaneti inayoanzia 1Mbps mpaka 21Mbps. Mteja anaweza kuchagua spidi kwa inayolingana na matumizi na kupunguza spidi ya intaneti, vivo hivyo kwa spidi ya kawaida ya Smile ya 21Mbps wakati wowote.

“Lengo la Smile ni kuwasaidia wateja kutumia intaneti kwa ufanisi,usahihi na kuepuka watu kutofahamu nini kinaendelea. Usimamizi binafsi wa matumizi ya vifurushi unalengo wa kuwasaidia wateja kudhibiti kupotea kwa data kusiko kwa lazima.” Akifafanua Bi. McGloin alisema“ Maelezo zaidi ya nini wanaweza kufanya kwa kila spidi yanapatikana kwenye mtandao wa Smile kama maelekezo.

Bi McGloin alifafanua “Matumizi ya mtandao wa 4G Tanzania yameongeza ufanisi wa watumiaji. Bidhaa zetu tangu tulipoanza mwaka 2012, zimeupa mtandao wa intaneti uhai wa Kasi zaidi unaotakiwa kwa wateja wetu. Kuperuzi intaneti, kuhamisha taarifa bila kukwama, mawasiliano ya simu kwa njia ya sauti au video ni hisia mpya na imekuwa bora zaidi, yaharaka, rahisi, nafuu na yakuaminika,”

Smile imefanya mapinduzi ya mawasiliano ya mtandao afrika mashariki ilizindua mtandao wa kwanza wa 4G. Mwaka mmoja baada ya huduma na maoni ya wateja, ujio huu mpya umeonyesha kuwa na mawazo mengi mapya na njia mpya za kuwapatia wateja wanachokihitaji. Uvumbuzi zaidi utegemewe kutoka Smile katika miezi michache ijayo na upanuzi wa mtandao mapema zaidi, hata watanzania zaidi kunufaika na huduma kutoka Smile.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: