Na Mwandishi Wetu

Bondia Imani Daudi anatarajia kupigana na Patrick Amote kutoka kenya kwenye mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi utakaofanyika katika ukumbi wa musoma bar Tandika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Nyerere Day tarehe 14 mwezi huu mpambano huo unaoratibiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO chini ya Rais wake Yassin Abdallah 'Osthadhi' lina marengo ya kumkumbuka baba wa taifa katika siku hiyo ya kipekee kabisa kwa nchi yetu ya Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Abdallah amesema kuwa kila mwaka wanafanya hivyo kwa ajili ya kumkumbuka baba wa taifa hili ambaye alipenda michezo mbalimbali bila ubaguzi wa aina yoyote hile ingawa kwa sasa michezo inabaguliwa kwa mingine kupewa ufadhili na mingine kupewa kidogo na mingine kunyimwa kabisa ufadhili

Aliongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mipambano mbalimbali ya utangulizi moja likiwa bondia Shomari Milundi atamenyana na Suma Ninja na mapambano mengine mbalimbali

Nae bondia Imani Daudi amejidhatiti kufanya kweli kwa kumsambalatisha Amote wa kenya ili aendeleze wimbi lake la ushindi na kuvutia mashabiki zaidi katika mchezo huo wa masumbwi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: