Kati kati ni Bwana na Bibi Denis (Nasibu) Msaki wakiwa na wasimamizi wao katika harusi yao takatifu iliyofungwa katika kanisa la Roman Katoliki parokia ya Mavurunza Kimara jijini Dar es salaam.
Maharusi Denis na Siael wakimtanguliza Mungu kabla ya kuanza kwa sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Green leaf Kimara Korogwe.
Bwana na Bibi Denis (Nasibu) Msaki siku ya jana ya tarehe 20/09/2014 ndio siku yao ambayo walikuwa wanaisubiri kwa muda mrefu baada ya kutimiza ndoto yao katika uchumba wao na kufunga ndoa takatifu katika kanisa la Roma parokia ya Mavurunza Kimara jijini Dar na baadae ikafuatiwa na sherehe ya nguvu iliyofanyika katika ukumbi wa Green leaf uliopo Kimara korogwe jijini Dar es salaam. Sherehe hiyo iliongozwa na MC msanii maarufu wa maigizo Bwana Novatus Michael anayejulikana kwa jina la kisanii kama Nova
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: