Baadhi ya wadau na wapenzi wa filamu wakitazama filamu ya ‘Samaki Mchangani’ iliyoandaliwa na muongozaji filamu mtanzania Amil Shivji kutoka Kijiweni Prductions wakati wa uzinduzi wa maonesho ya filamu ya Kiafrika Arusha (AAFF) New Arusha Hotel jana. Maonesho hayo ya wiki nzima yapo chini ya udhamini wa Tigo.
Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Kaskazini David Charles akizungumza na wadau wa filamu (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa simulizi za Kiafrika kupitia filamu na mchango wake katika kukuza utamaduni wa Kitanzania hususan lugha ya Kiswahili kwa upande wa Tanzania na Afrika Mashariki.
 Kikundi cha ngoma kinachoitwa ‘AfriCulture Group’ kikitoa burudani wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo ya wiki nzima jijini Arusha yaliyodhaminiwa na Tigo.
Wapenzi wa filamu wakifuatilia ratiba kwa karibu.
Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Kaskazini David Charles (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa filamu kutoka nchi za Rwanda, Burundi, Misri na Nigeria wakati wa uzinduzi wa maonesho ya filamu ya AAFF jijini Arusha yaliyo chini ya udhamini wa Tigo
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: