Mustapha Said Toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est akiwakaribisha wageni waalikwa kwenda kwenye meza kuu kujione kwa macho ni namna gani bidhaa zao zinavyofanya kazi.
Na Mwanishi Wetu.
Kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Juzi imetambulisha Aina Mpya Ya Tiles kwenye soko la Tanzania ikiwa na kauli ya "SURE STEP" ndani ya Hotel ya Double Tree Jijini Dar es Salaam..Aina mpya hiyo ya Tiles ni mpya Tanzania kwani ni aina ambayo haina utelezi wakati wote hata pindi ikiwa na maji au Imelowa kwa Mvua au Unyevunyevu.Sure Step inafanya Kazi Vipi?akiongea na wageni walioalikwa na wadau mbalimbali Bwana Thomas amesema kuwa Tiles Hizo zina ubora wa hali ya juuu ikiwemo Garantii ya Mwaka Mmoja mpaka Mitatu.Pia akaongeza Tiles hizo pindi zitumikapo haziwezi kuharibu sakafu wala kuweka nyufa,pia ni rahisi kusafisha pindi tu zinapochafuka kwani zimetengenezwa kwa mfumo ambao haziwezi kunyonya uchafu wa aina yoyote ile.Bwana Thomas akaongeza kuwa pia Bidhaaa hiyo ni rafiki wa mazingira kwani haina aina yoyote ya kemikali na pina zinaweza kutumika kwa matumizi ya ndani na nje.Aina za Tiles zilizotambulishwa jan ni pamoja na Stay Clean NS30,Stay Clean NS60 na Stay Clean NS90.
Bwana Thoma alisisitiza kuwa nia ya kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est kutambulisha Tiles hizo Nchini ni kuongeza Usalama wa watumiaji wa maeneo mbali mbali ikiwemo Hoteli,Migahawa,Mjumbani,sehemu za Burudani na Maofisini Bwana akatoa mfano kuwa Nchini Canada kumekuwa na kesi nyingi za watu kuvunjika miguu kupata maumivu kutokana na matumizi ya Tile ambazo zina utlezi Pindi tu zipatapo maji Au unyevu,Hivyo akatoa uwito kwa makampuni mbalimbali ya Ujenzi Tanzania na Nje ya Tanzania kutumia Bidhaa zao ambazo ni salama na rafiki kwa matumizi ya Binadamu.
Wageni waalikwa na Wadau wakiendelea kufuatilia
Wadau mbalimbali wakiwa makini kusikiliza na Kusoma kila kilichokuwa kinaelezwa na Mr Thoma toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Jana Kwenye Hoteli ya Double Tree Jijini Dar.
Mr Thomas toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est akionyesha mfano wa kitambaa ambacho ukimagia maji hakilowi wala kushika maji ikiwa ni kuelezea namna bidhaa zao zilivyo
Mr Thoma toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Akiwanyesha kwa vitendo wageni waalikwa na wadau mbalimbali namna bidhaa zao zinavyofanya kazi kwenye mazingira tofauti.
Wageni waalikwa Wakiendelea kupata maelezo na kuuliza maswali kwa Bwana Thomas toka kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est jinsi bidhaa zao zilivyo na zina ubora gani.
Maelekezo yakiendela toka kwa Bwana Thomas kwa wageni mbali mbali.
Wakurugenzi wa kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est Toka Kushoto ni Chair Woman Khadija Naif Alyafa akifuatiwa na Mustapha Said,Nala Nait Alyafa(Director) na Wa Mwisho Kulia ni Naji Ahmed.
Wadau wakijalibu kukanyaga Tiles na Kuona kama Zinateleza ama Vipi ndani ya Hoteli ya Double Tree Jijini Dar wakati wa utambulisho wa Tiles Mpya Toka Kampuni ya Canadian Solution Trading&Cleaning Est.
Toa Maoni Yako:
0 comments: