DSC_0034

Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushiriki wao kwenye zoezi la kusafisha mazingira yanayozunguka fukwe za bahari ya hindi kata ya Kivukoni lililokuwa likiendeshwa na kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd. Katikati ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena na Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.


Na Mwandishi wetu.

KAMPENI kubwa ya kuhamasisha usafi iliyokuwa inaendeshwa kampuni ya Green Waste Pro Ltd katika kata tatu za katikati ya jiji imemalizika kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kufanya eneo hilo kumeremeta tena.

Kampeni hiyo ambayo ilianza Septemba 6 mwaka huu ilifungwa kwa usafi katika kata ya Kivukoni ambapo kampuni ya TICS ilishiriki kufanya usafi katika fukwe za bahari.

Katika kampeni zilizoshirikishwa wadau mbalimbali wa mazingira na afya katika kuhamasisha usafi miongoni mwa wananchi pamoja na kufanya usafi viongozi walitumia nafasi hiyo kufunza watu umuhimu wa kushiriki katika kufanya usafi na kuwa wasafi.

Kata zilizohusika na kampeni hiyo ni kata ya Kisutu, Mchafukoge na Kivukoni.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa alisema usafi huo umelenga kuweka maeneo ya bandari kuwa masafi na japokuwa wao wapo Temeke waliona kuna kila sababu ya kushiriki usafi kwenye maeneo ya bahari ambayo wanafanyia kazi.

Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu alisema kampeni hiyo ambayo imefanikiwa, ilikuwa inawakumbusha wananchi wajibu wa kushiriki katika kuweka maeneo safi .
Baadhi ya wafanyakazi Kampuni ya Kupakua na Kupakia Kontena Bandarini (TICTS) wakifanya usafi kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo Kata ya Kivukoni kwa ajili ya kushiriki zoezi la kusafisha fukwe hizo katika kuhitimisha kampeni usafi iliyokuwa ikiendeshwa na Kampuni ya Green Waste Pro Ltd mwishoni mwa juma.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TICTS na Green Waste Pro Ltd wakishirikiana kusafisha fukwe za bahari ya hindi wakati wa kuhitimisha kampeni ya usafi iliyokuwa ikiendeshwa na Green Waste Pro Ltd.
Umoja ni Nguvu...... wafanyakazi wa kampuni ya TICTS wakizoa uchafu uliopo pembezoni mwa fukwe hizo wakati ambao wakati mwingine unapelekea kutoa harufu mbaya kwenye maeneo hayo.
Maji taka yanayoingia bahari ya hindi toka maeneo ya jiji la Dar es Salaam.
DSC_0151
Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima (kushoto) akishiriki zoezi hilo na wafanyakazi wenzake wa kampuni hiyo.
Usafi ukiendelea.

DSC_0096
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (kulia) akivaa glovu tayari kushiriki zoezi la kusafisha mazingira yanayoizunguka bahari ya hindi katika Kata ya Kivukoni mwishoni mwa juma. wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa TICTS.
Picha za pamoja baada ya kazi.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Meneja uhusiano wa TICTS, Jema Kachota pamoja na wafanyakazi wenzao wakipata ukodak baada ya kazi.
Pichani juu na chini ni timu za vitengo mbalimbali kutoka kampuni ya TICTS katika picha ya pamoja kabla ya kucheza mechi ya ndani ikiwa ni kusheherekea kuhitimisha kampeni ya usafi iliyokuwa ikiendeshwa ndani kampuni yao kwa takribani wiki nzima na kuamuua kuwaunga mkono kampuni ya Green Waste Pro Ltd ambayo nayo pia ilihitimisha kampeni zake za usafi zinazoendeshwa kila mwaka.
Mtanange ukiendelea.
Ilikuwa ni piga nikupige.
Meneja Kitengo cha Makontena TICTS, Bw. Donald Talawa (katikati) akitimua vumbi kuwania mpira wakati wa mechi za kirafiki baina ya vitengo vya kampuni ya TICTS.
Kila mmoja akionyesha ufundi wake wa kupiga kanzu.
Mfanyakazi wa TICTS akila tizi ili aingie uwanjani.
Vumbi likiendelea kutimka wakati wa mechi za ndani za vitengo vya kampuni ya TICTS katika kusheherekea kuhitimisha kwa kampeni ya usafi iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro Ltd.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. thanks bro for the snap umetuwakilisha ile ile ,respect

    ReplyDelete