Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akimkabidhi nahodha wa Mkolani Fc Meck Lyimo, kombe la ubingwa wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 mara baada ya timu hiyo kuifunga timu ya kata ya Mirongo bao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jumamosi uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na kuhudhuriwa na mashabiki wengi.
|
Kikosi cha timu mabingwa Mkolani Fc katika picha ya pamoja kabla ya kuvaana na Mirongo Fc kwenye mchezo wa fainali Pepsi Kombe la Meya 2014 uliochezwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. |
|
Kikosi cha timu Mirongo Fc katika picha ya pamoja kabla ya kuvaana na Mkolani Fc kwenye mchezo wa fainali Pepsi Kombe la Meya 2014 uliochezwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. |
|
Ni wakati wa kupata mawaidha toka meza kuu ya wageni na wenyeji wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ambayo mwasisi wake ni Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula. |
|
Balozi wa habari wa Pepsi Albert G. Sengo (katikati) akitoa utangulizi kuhusiana na Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014, mbele ya meza kuu. |
|
Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa, (mbele) akiongoza msafara wa Meza kuu kukagua timu kabla ya mchezo wa fainali kuanza,nyuma yake ni muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Meneja wa Kampuni ya SBC Nicolous Coertz. |
|
Mashabiki wakifuatilia kwa ukaribu michuano hiyo. |
|
Muasisi wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya, Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akizungumza na mashabiki wengi waliofurika katikauwanja wa Nyamagana kushuhudia fainali hizo, ambapo hadi mwisho timu ya kata ya Mkolani waliibuka Mabingwa kwa kuifunga Mirongo Fc 2-1. Katika Picha anaonekana Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (wa pili toka kushoto) Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa (kushoto) na Meneja wa Kampuni ya SBC Nicolous Coertz (kulia). |
|
Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa naye alipata nafasi ya kuzungumza na wana Mwanza. |
|
Meneja wa Kampuni ya SBC Nicolous Coertz naye alipata nafasi ya kuzungumza ambapo aliwateka mashabiki kwa kuitumia vyema lugha ya kiswahili. |
|
Kundi la sanaa Bujora Dancing Group lilisababisha burudani nyingine ya mvuto. |
|
Burudani ilikolea macho mbeeeele kwenye tukio. |
|
Kila mtu na nafasi yake macho kwenye mchezo. |
|
Mkolani Fc wakitoka kushangilia goli la kwanza lililofungwa kipindi cha pili na Siraji Juma. |
|
Hii ni moja kati ya zawadi za mshindi wa kwanza ambapo mbali ya kupata Kombe, fedha taslimu shilingi milioni 1.5, na medali ya dhahabu vilevile bingwa wa michuano hiyo aliondoka na Bajaji hili lenye tahamani ya shilingi milioni 4.5 |
|
Mkolani Fc wakishangilia bao la pili na la ushindi lililofungwa na Paul Godfrey. |
|
Mashabiki wa Mkolani wakiwa wamembeba kocha wa timu yao mara baada ya mchezo kumalizika wakiwa na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mirongo Fc. |
|
Zawadi ikiwa chini ya ulinzi. |
|
Mwamuzi Bora wa Mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ni David Albert. |
|
Wafuatiliaji aka mashuhuda. |
|
Mwamuzi Bora wa Mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ni David Albert, akishangilia mara baada ya kukabidhiwa kitita cha shilingi laki mbili, aliyekabidhi ni diwani wa Kata ya mirongo mhe. Mkama. |
|
Meneja wa SBC watengenezaji wa vinywaji vya Pepsi Nilolous Coertz (Kushoto) akimkabidhi fedha taslimu shilingi laki mbili na kiatu cha dhahabu mfungaji bora wa mashindano Paul Godfrey wa Mkolani Fc aliye kuwa na magoli nane (8) |
|
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida akikabidhi kombe la mshindi wa tatu kwa timu ya Sokoni Fc. |
|
Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa akikabidhi kombe kwa washindi wa pili wa Pepsi Kombe la Meya 2014 timu ya Mirongo Fc, ambapo pia aliwakabidhi kitita cha shilingi milioni mbili taslimu. |
|
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akimkabidhi funguo na vidhibitisho vyote vya zawadi ya gari la mizigo Bajaji kwa ajili ya kuanzisha ujasiliamali, na mpokeaji ni Nahodha wa timu mabingwa Mkolani Fc Meck Lymo. |
|
Wacha shangwe zitawale. |
TIMU ya Kata ya Mkolani FC imeibuka mabingwa wapya wa Kombe la Meya 2014 baada ya kuichapa timu ya Kata ya Mirongo bao 2-1 juzi katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Awali katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ulioanza mapema saa 8:00 mchana kwa timu ya Sokoni FC kuichapa Mnadani FC bao 3-0na kuibuka mshindi wa tatu wa michuano hiyo huku magori ya Sokoni yakifungwa na Joseph Mwajalila dakika 33 kwa penati na Salimu Hamis dakika 39, 51na kuwapa tiketi ya ushindi wa tatu.
Fainali hiyo iliyoshuhudiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TFF Selesitine Mwesigwa, muasisi wa mashindano hayo Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza, Stanislaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hida, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Mwanza (MZDFA), Jackson Songola na Katibu wa MZDFA, Nasibu Mabrouk.
Ndikilo amesema mashindano hayo yamewezesha vijana kuonyesha vipaji vyao, hivyo ni vyema sasa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakawatumia vijana walionesha uwezo kuunda timu ya Mwanza City FC kama ilivyofanya Jiji la Mbeya.
“Ni bora mkaunda timu ya Mwanza City FC ili kushiriki ligi na huenda ikatinga ligi kuu Bara kama walivyofanya wenzetu wa Mbeya na sasa timu ya Mbeya City FC inashiriki ligi kuu, kwani timu zetu kongwe katika Mkoa huu za Toto FC na Pamba FC zimeonekana kuishiwa mbinu na kufanya vizuri ili kurejea ligi kuu,”alisema.
Katika mchezo huo mkali wa vuta ni kuvute kilishuhudia timu hizo zikienda mapumziko zikiwa hazijafungana na kipindi cha pili mchezaji Siraji Juma aliwainua mashabiki kwa kuandika bao la kwanza na bao la pili likifungwa na Paulo Godfrey huku katika hekaheka ya kuokoa mpira ulioelekezwa langoni mwake akijikuta akijifunga na hadi mwisho wa mchezo wadau wa michezo walishuhudia timu ya Mkolani ikitangazwa kuwa mabingwa kwa kuinyuka Mirongo Fc bao2 - 1.
Mashindano hayo ya kombe la Meya 2014 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya kutengeneza vinywaji vya Pepsi (SBC), Ndikilo alikabidhi bingwa timu ya Mkolani FC zawadi ya kombe, fedha tasilimu Sh milioni 1.5, medali ya dhahabu na Bajaji ya mizigo yenye thamani ya Sh milioni 4.5, mshindi wa pili alinyakuwa Sh milioni 2, kombe dogo na medali ya fedha.
Timu ya Sokoni FC iliyoibuka mshindi wa tatu ilijinyakulia fedha tasilimu Sh milioni 1, medali ya shaba na kombe dogo, mfungaji bora Paulo Godfrey akiwa na bao nane na kunjinyakulia kiatu cha dhahabu na Sh laki mbili, mwamuzi bora kutoka Kituo cha Alliance ilichukuliwa na David Albert na kupata Sh laki mbili huku timu ya Kata ya Mahina FC ikipata Nidhamu bora na Sh laki mbili.
PICHA/HABARI NA GSENGO
Toa Maoni Yako:
0 comments: