Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai (Kati kati)akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kibaigwa. Hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo umefanyika jana katika viwanja vya Tawi la NMB Kibaigwa Wilaya ya Kongwa mkoni Dodoma.Wakishudia uzinduzi huo ni Bw.Ole Loibanguti , Meneja wa NMB kanda ya kati ( Kulia) na mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe.Alfred Msovera.
Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kibaigwa. Hafla ya uzinduzi wa Tawi hili umefanyika jana katika viwanja vya Tawi la NMB Kibaigwa Wialaya ya Kongwa mkoni Dodoma.Akishudia uzinduzi huo ni Bw. Ole Loibanguti ,Meneja wa NMB kanda ya kati ( Kushoto) NMB leo imefungua tawi jipya katika mji maarufu wa Kibaigwa –Dodoma. Tawi hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya NMB nchini kote.
Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Mhe.Job Ndugai akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni mara tu baada ya uzinduzi wa Tawi la NMB Kibaigwa.
Wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
Picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa Tawi.
---
Na Mwandishi Wetu.

Tawi la Kibaigwa limefunguliwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, Mh Job Ndugai.

Kufunguliwa kwa tawi la Kibaigwa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wa NMB wa eneo hilo wa kupata tawi lenye nafasi ya kutosha .Aidha eneo hili ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wakubwa wa NMB na wananchi kwa ujumla.

Kwa kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za kijamii, benki ya NMB inatoa shilingi Milioni 10 kwa ajili ya hospitali na shule kama shukrani za Benki kwa wananchi wa Kibaigwa kwa kuendelea kwao kuunga mkono maendeleo ya benki.

NMB ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 150, ATM Zaidi ya 500 nchi nzima pamoja na idadi ya wateja inayofikia Milioni mbili hazina ambayo hakuna benki yenye nayo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: