Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakishiriki katika  michezo  wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Kema Mabango, Abdallah Gunda na Jackson Mmbando wakishiriki katika shindano la kukuna nazi wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam.
Washindi wa shindano la kukuna nazi wakishow love. Kutoka (kushoto), Mshindi wa Kwanza, Abdallah Gunda, Mshindi wa Pili, Jackson Mmbando na Mshindi wa Tatu, Kema Mabango.
Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakiogelea wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Wafanyakazi wa Airtel na familia zao wakijisevia maakuli.
 Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) akiwahudumia chakula wafanyakazi wa Airtel na familia zao.

• Airtel Family day yalenga kuongeza hamasa kwa wafanyakazi kujituma katika kazi zao Imeelezwa kuwa ufanisi wa watumishi katika ngazi mbali mbali za kiutendaji unaweza ukaongezeka pindi wafanyakazi wanapokutana pamoja na kubadilishana mawazo na viongozi wao katika hali ya kiurafiki.

Akizungumza katika tamasha la siku ya familia ya kampuni ya simu za mkononi ya airtel, Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo SOPHIA MELAMALI, amesema kuwaweka wafanyakazi katika eneo moja na familia zao kunadumisha mshikamano baina ya wafanyakazi  na familia zao kitendo kinachoongeza ufanisi katika eneo la kazi.

“Airtel tumejipanga kuwa na muundo mzuri wa kufurahia matunda ya kazi yetu na falilia yetu kwa kuwa hii inasaidia sana kuwafanya wafanyakazi wetu kukutana, kufahamiana na kufurahi na familia zao  na hatimae kupunguza msongo wa mawazo ya kawaida ili kuendelea kufanya kazi ya kuhudumia wateja wetu vyema” alisema SOPHIA MELAMALI Meneja Rasilimali Watu Airtel.

Nao baadhi ya wafanyakazi wa airtel wamepongeza kitendo cha kampuni hiyo kuandaa tamasha hilo na kubainisha kwamba ni sehemu ya kuwawezesha wafanyakazi kufahamiana.

Wamesema tukio hilo linawawezesha wafanyakazi kupumzika na familia zao pamoja na wafanyakazi wenzao katika mazingira tulivu na a kirafiki ADRIANA LIAMBA Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Airtel sisi wafanyakazi wa Airtel  tumefarijika sana na jinsi ambavyo leo uongozi na kampuniyetu ilivyotukutanisha na familia zetu zote ili tuweze kufurahia, hii pia inatupa moyo wakuendelea kuwahudumia wateja ipaswavyo na pia kushiki katika mambo ya kijamii zaidi kwa kuziona fulsa zilizomo leo na baadae”

“Mfano familia zetu tumekutana watu wa aina tofauti zikiwa na wafanyakazi wa baadhi ya mashirika mengine nchini, hii pia ni fulsa kwetu kuendelea kutengeneza wateja tutakaowahudumia kwa sasa au kuwekeza kwa watoto wetu ili waje kuwa wateja wa baadae,  kwa kweli family day party ni nzuri” alimaliza kwa kusema Bi Lyamba.

Baadhi ya watoto walioshiriki katika tamasha hilo ANTHONY NABOLI na FRANCIS ALEXANDER hawakusita kuonyesha hisia zao baada ya kucheza michezo ya aina mbali mbali kwa kuwashuru sana wazazi wao kwa kuwawezesha wao kushiriki michezo mingi katika viwanja vya FUN CITY pamoja na kupewa zawadi nyingi.

Nae afisa rasilimali watu wa Airtel na mratibu wa Family party hiyo Bw, Mubaraka Kibarabara alisema “tamasha letu la familia mwaka huu limekuwa na mafanikio makubwa hasa kwa kuwapa nafasi wafanyakazi siku nzima wakicheza michezo mbalimbali na kufurahi ikiwemo ile ya kuvuta

Kamba, kuimba karioke, kuogelea, kubembea katika mashine za kisasa, na kuwepo kwa shindano la kipekee kabisa lililovuta hisia za wengi la  wanaume kushindana kukuna nazi
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: