Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Rashid Mpinda.  Msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika  tamasha la Pasaka na Krismasi. (Picha na Francis Dande)
Watoto wa kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho, Halima Ramadhan wa tatu kulia.
Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Mwandaliwa cha Mbweni nje Kidogo ya jijini la Dar es Salaam.
Msama akiwa amembeba mtoto anayelelewa katika kituo cha Tovichodo cha Temeke.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama (lushoto),
akimkabidhi sehemu ya msaada wa vyakula Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto
wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Rashid Mpinda.  Msaada huo wenye thamani ya sh.
milioni 7 unatokana na mapato yaliyopatikana katika  tamasha la Pasaka na Krismasi.
 Katibu Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto
wanaoishi katika mazingira magumu cha Maunga Center cha Kinondoni jijini Dar es
Salaam, Rashid Mpinda akimshukuru Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama kwa misaada aliyotoa.
Watoto wakimshukuru Msama baada ya kuwapatia msaada wa vyakula mbalimbali.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Tovichodo cha Temeke, Honoratha Michael akipokea sehemu ya msaada wa vyakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama.

Na Francis Dande 

KAMPUNI ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, juzi ilitoa misaada ya kiutu kwa vituo vitatu vya kulea yatima vya wilayani Kinondoni na Temeke.

Msaada huo ambao ni utekelezaji wa programu ya kampuni hiyo kama moja ya kurejesha sehemu ya faida itokanayo na uratibu wa matamasha ya muziki wa injili kwa jamii.

Msama Promotions Ltd ambayo pia ni waratibu wa tamasha la muziki wa injili la Pasaka
na Krismas, si mara ya kwanza kwao kutoa misaada ya aina hiyo kwa vituo vya yatima na watu wengine wenye mahitaji kama wajane na wazee.

Vikundi vilivyonufaika na msaada huo Jumapili, ni kituo cha Kulea Watoto Yatima  cha Mwandaliwa cha Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na Maunga pia cha Kinondoni.

Aidha, misada hiyo imewafariji watoto yatima wa kituo cha Tovichido cha Wilayani
Temeke akisema amefanya hivyo baada ya kuguswa na hali halisi inayowakabili.

Msama alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa watu wenye uwezo, makampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii  kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.

Kwa upande wa misaada iliyokabidhiwa kwa vituo hivyo, ni mchele, sukari, unga,
mafuta ya kula, chumvi, unga wa ngano na vingine vingi kwa ajili ya matumizi ya kila siku nyumbani, vyote vikiwa na thamani ya shilingi mil 7.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Katibu wa Kituo cha  Maunga, Rashid Mpinda   alitoa pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo na kuwasihi wengine waige mfano huo wa kusaidia makundi maalum.

Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mpinda alisema ni kukosa uwezo wa
kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma hadi kufukuzwa kwa kukosa karo, hivyo
kushindwa kupata elimu.

Msama kwa upande wake alisema jukumu la karo za wanafunzi hao analibeba yeye pamoja na sare  kutokana na kuguswa kwake na kilio cha watoto hao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: