Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya kufua umeme ya Pan African Power Solution inayoimiliki kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imezidi kung’aa katika nchi za jumuia ya Afrika Mashariki katika kusambaza nishati ya umeme.
.
Hatua hiyo inasababishwa na serikali ya Kenya kuipatia barua kampuni hiyo ya kufanya nao kazi ya usambazaji umeme katika mradi unaohusisha nchi mbili za jumuia hiyo, ambazo ni Tanzania na Kenya.

Barua ya Kenya iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli, Injinia Joseph .K. Njoroge ya tarehe 19, Agosti 2014 kwenda kwa Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Sing Sethi.

Taarifa zaidi kuhusiana na barua hiyo, yenye kumbukumbu namba ME&D/CONF/3/2/73A iliyokuwa na kichwa cha habari Expression of interest for IPP for 2000MV power generations and supply to Kenya and Tanzania.

Barua hiyo, ilieleza kuwa inazitaka pande tatu hizo ikiwemo PAP, Tanzania na Kenya kukutana haraka kuona ni namna gani uzalishaji huo utaanza haraka iwezekanavyo.

Akithibitisha barua hiyo, Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema kampuni yao inaendelea kuchapa kazi na haitishiki na kauli za wanasiasa kwa kuwa wao si wanasiasa.

‘’Tunafurahi kuwa tunazidi kuaminiwa na serikali mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Hii inadhirisha ufanisi na ueledi wetu katika tasnia nzima ya nishati,’’alisema.

Hivyo, alisema anaamini maneno yote yanayoenezwa juu yao kuwa yanatawaliwa na chuki na wivu wa kibiashara kutoka kampuni zingine za usambazaji wa umeme.

Kutolewa kwa barua hiyo kwa IPTL kutaweza kuondoa sintofahamu iliokuwepo, baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR- Mageuzi) kudai kuwa Seth anayeongoza kampuni hiyo amepigwa marufuku kufanya biashara ya aina yoyote Kenya.

Kafulila alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini hapa, kuwa Seth ni fisadi na kwamba Kamati ya Bunge ya nchini Kenya imempiga marufuku kufanya biashara nchini humo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: