Dalili karibu zote zilizotajwa ni kama zimetimia hivi lakini Yesu hajarudi, WHY?

1.  Walokole Tumejichanganya, Kanisa limeshindwa kueleweka lina mishemishe gani na kujenga ufalme, Wachungaji wako bize kupiga Sadaka kuliko kupiga Injili watu waokoke... Ukiona wachungaji wanapigana vijembe hadharani unajua tu wote wanagombania Mtonyo, na main purpose ya KANISA imetoweka, Kanisa imekuwa SACCOSS, Yesu kila akichungulia dirishani hali hairuhusu..

2.Walokole tumezi-categorize dhambi,zingine zimebadilishwa na kuwa Vijidhambi huku dhambi zingine zikiwa MIDHAMBI MINENE..Mlokole yuko bize kumsengenya Mlokole mwenzie kisa Amezini,kwa sababu yeye alitoa mimba bila kujulikana na mtu lakini ni wa kwanza kumsema kwanini Kiongozi wa Praise and Worship amepata Mimba kabla ya ndoa..Yupi yuko sahihi??Aliyepata Mimba akaacha azae au aliyeua Mtoto bila kujulikana na kuonekana Bikira kumbe Kimeo??Yesu kila akichungulia dirishani hali hairuhusu

3.Walokole wanaundiana Magroup ya Whatsapp na Facebook kuwasema wengine,badala ya kumfuata na kuongea nae kama Mkristo mwingine..Ukishamsema Whatsapp UMEMSAIDIA NINI??Kwa kumsimanga Mlokole mwenzio unadhani wewe utaingia mbinguni kwa mlango upi??
Msengenyaji na Mzinzi WOTE WANAENDA MOTONI
Mfiraji na Muongo WOTE WANAENDA MOTONI
Mnafiki na Muuaji WOTE WANAENDA MOTONI

4. Hakuna Tofauti ya MLOKOLE na ASIYE MLOKOLE....Ni rahisi kusema Umeokoka mdomoni lakini Mwaitege alishaimba, tazama MATENDO... Wote tunaenda kanisani Jumapili, MLOKOLE anaenda Fellowship Jumatano na Maombi ya Tehillah Ijumaa, ila ASIYE MLOKOLE yeye kaishia Jumapili tu Ibada inamtosha... Mkiwa IGO LOUNGE Mlokole anaagiza NDOVU na Asiye Mlokole anaagiza HEINEKEN... Tofauti ya Mlokole na Asiyeokoka ni kwamba yeye haji Fellowship wala Maombi zaidi ya Ibada Jumapili..Ila Bia mnakunywa wote.. Uzinzi mnafanya wote... Majungu na Kusengenya mnafanya wote..Haoni UTOFAUTI...Utamshawishi kipi?? Utamwambia aokoke ili iweje wakati wote mnaishi SAME LIFE?? ili uwe na impact ni lazima kuwe na DIFFERENCE na kwa maisha ya sasa Walokole hatuonyeshi UTOFAUTI HUO na hivyo ni ngumu kumshawishi asiyeokoka aokoke maana haoni reason..
Yesu akirudi Leo GHAFLA Tutakaoenda Mbinguni hatujai hata BAJAJ 3. Tunajidanganya tu na maisha feki ya Kupretend tunayoishi huku tukiwa Bize kunyooshea wengine vidole wakati unajijua wewe ni Mchafu pia sema HUJULIKANI TU... Yesu anachelewa kutufanyia FAVOUR tu ili tubadilike....Mzinzi na Msengenyaji wote LAO MOJA!
Ziwa la Moto... Tusisahau hilo!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

4 comments:

  1. You real touch me! It's true a lot of us, we will go 2 Jehanum.

    ReplyDelete
  2. A Very, very nice message, ni ukweli mtupu siongezi chochote full stop.

    ReplyDelete
  3. kwa kweli Mungu atusaidie, ni ukweli mtupu.

    ReplyDelete
  4. kwa kweli Mungu atusaidie, ni ukweli mtupu.

    ReplyDelete