Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

UHIFADHI wa mazingira ni moja ya hatua muhimu kutokana na kuwa rasilimali ardhi ndio nguzo kuu katika maendeleo ya nchi mbalimbali kote ulimwenguni.

Ili nchi iendelee, ardhi imepewa kipaumbele kwa kuwa watu waliopo wanahitaji rasilimali hiyo kwa shughuli mbalimbali zikiwemo ujenzi, kukata miti kwa ajili ya kuni, makaa, chokaa, uchimbaji mchanga na nyenginezo nyingi zenye umuhimu kwa mwanadamu.

Moja ya mambo yaiyonisikitisha leo ni kuona maji machafu yanayotoka hospitalini, majumbani kwa watu yote yanaingia bahari ya hindi. Si tu maji machafu bali maji hayo yanaambatana na kinyesi ikiwa ni pamoja na harufu kali sana.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona fukwe hii imekuwa ikitumika kwa watu kujipumzisha na wengine kuogelea jambo ambalo kukweli ni hatari kwa afya. Hebu mtazamaji wa Kajunason Blog angalia video hiyo harafu utoe maoni yako.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: